Takriban mahujaji 717 wamepoteza maisha baada ya kukanyagana karibu na mji mtakatifu wa kiislam, Mecca nchini Saudi Arabia.
Watu wengine 863 wamejeruhiwa kwenye tukio hilo lililotokea kwenye eneo la Mina, wakati ambapo mahujaji milioni mbili kutoka nchi mbalimbali duniani walikuwa kwenye siku ya mwisho ya Hijja.
Hilo ni tukio baya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha Hijja katika kipindi cha miaka 25.
Wakati wa Hijja, mahujaji walisafiri kwenda Mina, bonde kubwa lililopo kilomita tano kutoka Mecca, ili kwenda kurusha mawe saba kwenye nguzo za Jamarat.
Nguzo hizo zinaaminika kuwa sehemu ambayo shetani alimrubuni Nabii Ibrahiym.
Tukio hilo limetokea wiki chache tuu baada ya watu 109 kupoteza maisha baada ya kuanguliwa na cranes kwenye msikiti mkuu wa Mecca.