Ray Ampangishia Chuchu Hans Mjengo Mpya Kuwakata Watu Vidomo

Madai mazito! Staa wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ anadaiwa kuonesha jeuri nyingine ya fedha baada ya kumpangia mwandani wake, Chuchu Hans mjengo mpya wenye hadhi.

Ubuyu kutoka kwa mtu wa karibu wa mastaa hao ulinyetisha kuwa Ray alifikia hatua hiyo baada ya mkataba wa nyumba aliyopangishiwa Chuchu awali maeneo ya Mwanayamala-Kwamsisiri, Kinondoni jijini Dar kumalizika muda wake.
“Kwa sasa Chuchu haishi Mwananyamala. Ray amempangia mjengo mpya maeneo ya Sinza-Darajani (Dar).

“Unajua kule Mwananyamala mkataba uliisha na baby wake mtu alitaka kubadilisha mazingira ya kuishi, naona kaka mkubwa ameamua kumsogeza kwenye viunga vyake vya Sinza, nasikia ni mambo ya mahaba niue,” kilidai chanzo hicho.

Alipotafutwa Chuchu na kuulizwa kuhusiana na ishu hiyo alijibu kifupi:
“Jamani hizo ni personal issues (mambo binafsi) si lazima kila mtu ajue mimi ninaishi wapi.”
Kwa upande wake Ray simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea ili kusikia upande wake.

Source: GPL
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ujinga mtupu anaacha kumjengea kazi kupangishiana tu, mwisho wa siku waanze kutembeza vibakuli. mfyuuuu!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad