Kikwete |
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kutoa ufafanuzi kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili ya safari za Viongozi Wakuu yaani Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 kwa ajili ya Idara ya Itifaki. Kwa miaka mingine yote wastani umekuwa ni kati ya shilingi bilioni tano hadi 25 kulingana na mahitaji ya idara hiyo.
Ifahamike kuwa kiasi hicho cha shilingi bilioni 50 ni bajeti nzima ya Idara ya Itifaki, ambapo kuna fungu maalum kwa ajili ya ziara za viongozi. Fungu hilo linagharamia makundi makuu matano kama ifuatavyo:
1.Kundi la Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
2.Kundi la Makamu wa Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
3.Kundi la Waziri Mkuu wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
4.Kundi la Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nje ya nchi wanapotembelea Tanzania; na
5.Kundi la Wajumbe Maalum wanaokuja nchini kuleta taarifa muhimu kwa Rais.
Makundi yote haya hugaramiwa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ndani ya bajeti ya Idara ya Itifaki kifungu cha Ziara za Viongozi.
Aidha uandaaji wa bajeti ya Wizara chini ya Idara ya Sera na Mipango unahusisha wadau wengine nje ya Wizara kama vile Kamati ya Bunge ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hupitishwa kila mwaka na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunapenda kuwaatahadharisha wananchi juu ya watu wanaotoa taarifa za uongo kwa madhumuni ya kujenga chuki dhidi ya Serikali. Ikumbukwe kuwa ziara za viongozi zinazoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje zina mafanikio makubwa kwa nchi na Watanzania kwa ujumla.
Wizara inaandaa taarifa ndefu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara, changamoto na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambayo itatolewa kwa umma kwa lengo la kutoa elimu zaidi.
MWISHO.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
17 Septemba 2015
Ukweli uko wapi?Ilishtusha uma kwa kweli,hii inachanganya maana ni hela nyingi mno.
ReplyDeleteMzee CCM isije kufia mikononi mwako,tunaipenda bado.
HII NDIYO HALI HALISI.TAARIFA HII YA MHE.MBATIA SIO MPYA ILA IMEKUJA KWENYE SURA YA UKOMAVU WA TAKWIMU NA MABORESHO.KWA HILI PIA TUNAISUBIRIA KWA HAMU KUBWA KILE KINACHOITWA TAARIFA NDEFU YA WIZARA YA MAMBO YA NJE SASA HATUJUI KUMKANUSHA MBATIA AU KUSAHIHISHA TAKWIMU.OMBI;MSEMAJI WA WIZARA AENDE [KWENYE MAELEZO YAKE]KUFAFANUA SAFARI ZOTE ZA MHESHIMIWA TANGU ANAINGIA MADARAKANI 2005 HADI LEO 2015.RAIS WETU KAITUMIA KWELI KWELI HAZINA YA NCHI YAANI KWA LUGHA NYINGINE YA UWAZI HAKUWA NA HAJAWATENDEA HAKI WATANZANIA WALIO KWENYE DIMBWI KUBWA LA UFUKARA,LA UMASKINI WA KUTUPWA.NI DHAHIRI NA WAZI KABISA WATANZANIA TULIO WENGI TUMEKUWA TUNAKERWA SANA NA SAFARI ZISIZO NA ULAZIMA ZA RAIS WETU,NA,TUNAKUMBUKA KUNA NYAKATI ANASAFIRI NCHI IKIWA KWENYE MAJANGA MBALI MBALI.TRILLION NNE NI BAJETI YA NCHI YA MWAKA.TUNAHITAJI MAJIBU.NA,JAMBO HILI KWA KUWA NI KUBWA SANA NA LINAHUSU TAIFA NA UHUJUMU PATO LA TAIFA,JASHO LA` WALIPAKODI TUNAOMBA LIBEBWE NA WABUNNGE WETU WATAKAOFAULU KUINGIA BUNGENI NOVEMBA 2015 KAMA AJENDA YA MUHIMU ILI HATUA STAHIKI NA FUNDISHO ZIWEZE KUCHUKULIWA KWA MUJIBU WA SHERIA ZETU.SIKU ZOTE TUNAJIULIZA MAANA YA KUWA NA WASAIDIZI NI NINI? MAWAZIRI,MANAIBU,MAKATIBU WAKUU,WAKURUGENZI,MAKAMISHNA,WAKUU WA TAASISI NA WENGINEO WENGI.KWA KWELI INASIKITISHA,INAUMA,INAKATISHA TAMAA.KAMA UONGOZI NDIO HUO BASI TUJIHESABIE MKAO WA HASARA NA MAJANGA.MTU MMOJA TRILLION NNE[4]!
ReplyDeleteombi maalum kwa wagombea urais wetu wote wanane[8] .jee nani kati yenu yupo tayari akifaulu kuchukua nchi KUMFUNGA PAKA KENGELE? hili ni zito sana.mbatia kapewa takwimu sahihi toka jikoni.hali hii ya matumizi makubwa hivi ya mheshimiwa rais wakiipata wafadhili wetu wakuu yaani world bank,european union,marekani,nchi za scandinavia,japan,australia watatujadili kuifunga kabisa misaada waliyoikusudia hii ni pamoja na budget support 2015/2016.inatisha.trillion nne kwa safari za mheshimiwa rais hata marais 15 wa afrika hawawezi kufikia bajeti hiyo.kweli tumeliwa tena tumeliwa sana.inakatisha tamaa kabisa.
ReplyDeletesuali moja kuhusu mikataba ya kimataifa inayofikiwa na mataifa rafiki mbali mbali ni yeye mwenyewe mheshimiwa rais anasaini au ni mawaziri au wakuu wa taasisi au makatibu wakuu hususani katibu mkuu wizara ya fedha?kama ni mawaziri yeye anafanyaje pale?shuhuda au zipo hesabu nyingine tena?mikutano ya wakuu wa nchi sawa lakini anaambatana na akina nani.nadhani matatizo yanayohitaji kutatuliwa ndani ya nchi ni mengi mno kuliko kutamba anga za kimataifa kwa fungu la wizara ya fedha,linatoka wapi hilo fungu kama si fedha za mikopo zinazokusudiwa kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo?kumbe ndio maana neno uhaba wa bajeti linatawala.
ReplyDeletehii ni funga kazi ya harakati za kampeni ya uchaguzi mkuu wa tanzania 2015,funga kazi kwa sababu maelezo mazito niliyoyasoma hapo juu ni ya ukweli ya kina yanaleta hisia kali na uchungu mwingi kwa sababu upotevu huu wa makusudi wa trillion nne[4] hauvumiliki,ni mkubwa mno mno hii ni grand scandal,grand misappropriation wachanganye mwalimu,mwinyi na mkapa kwa pamoja hawafikii hesabu hii ya trillion nne.acha nne hata iwe moja,tusiliachie hili bila hatua.tushikamane watanzania
ReplyDelete