Siri Nzito Yafichuka Kuhusu Mastaa Kuhama Kutoka Ukawa Kwenda CCM

Mwigizaji wa tasnia ya filamu nchini, Aunt Ezekiel, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Kajala Masanja Kay’ wakiwa CCM. Stori: Na Erick Evarist
NYUMA ya wimbi kubwa la mastaa waliokuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuna siri nzito zilizojificha na Amani limechimbua kutoka kwa wahusika.
Aunt Ezekiel na Vincent Kigosi ‘Ray’ walipokuwa Ukawa.Hivi karibuni, mastaa mbalimbali akiwemo mwigizaji Aunt Ezekiel na Vincent Kigosi ‘Ray’ waliokuwa wakishabikia Chadema kinachoungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walitangaza kuhamia CCM na kuzua taharuki kwa wafuasi wao.

Baada ya wawili hao kuhamia CCM, yaliibuka madai kuwa wamehongwa mamilioni ya shilingi ili waachane na Ukawa na wahamie CCM.
“Hawana lolote tunajua wamehongwa fedha na CCM ili waikane Ukawa, njaa hizi zitatuua jamani,” yalisomeka madai hayo katika mitandao mbalimbali.

Mwanahabari wetu baada ya kushuhudia madai hayo yakizidi kusambaa mitandaoni, kwa nyakati tofauti aliwapigia simu Ray na Aunt ambao kwa pamoja waliyakana na kuwataka Watanzania kusikia siri iliyowafanya wao kushtuka na kuhamia CCM.
“Jamani niwaambie ukweli, sijahongwa na chama chochote. Nimetafakari kwa makini na kuamua kuhamia CCM kutokana na ukweli ndiyo chama kilichotufikisha hapa tulipo na kinachoweza kutufikisha mbali zaidi.

“Ninawashangaa wanaozungumzia kuwa tumehongwa ili tuhamie CCM, mbona hawasemi Edward Lowassa na Fredrick Sumaye (mawaziri wa zamani-CCM) wamehongwa kuhamia Ukawa?
“Nisiwafiche, nafsi ilikuwa inanisuta sana kuwa Ukawa. CCM ndiyo kila kitu, maendeleo ya kweli yanaletwa na mtu anayezungumza sera na kumaanisha kile anachozungumza, CCM wamesimamisha mgombea ambaye hata kama wewe ni mpinzani utakubali tu ni mchapakazi.

“Niwasihi vijana wenzangu kujitambua, kusikiliza sera za wagombea wote na kufanya uamuzi sahihi, wasisukumwe na mhemko tu inayohusishwa na mabadiliko. Wampime mgombea anayehubiri mabadiliko anamaanisha?”

Kwa upande wake Aunt alisema: “Kwanza nikatae sijapewa hata shilingi na CCM. Kilichonihamisha Ukawa ni sera na Ilani. Sera na Ilani ya Chadema haizungumzi moja kwa moja kumkomboa Mtanzania wa hali ya chini.

“Wanahubiri mabadiliko tu bila kueleza watayaletaje? Busara wala kusisitiza amani hakuna. CCM ina sera na Ilani inayotekelezeka. Nimeilewa ndiyo maana nikaamua kuunga mkono. CCM ina viongozi waadilifu, wenye hofu ya Mungu, wasiokuwa na tamaa ya madaraka tofauti na wale wa Ukawa.
“Niwaase vijana na Watanzania wote ambao bado hawajashtuka, washtuke na kuja CCM ambako kunaeleweka.”
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ikowapi hio siri nzito,kweli udaku ni udaku,pesa wamepewa Lkn hawawezi kukubali hadharani km wamepewa pesa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na walivyokuwa UKAWA walipewa pesa?fyuuuuuuuuuuuuuuuuu

      Delete
  2. Magwanda na Kijani wapi na wapi hata muonekano wa Kijani unavyopendeza unakupa ishara ya mafanikio

    ReplyDelete
  3. Nawashangaa sana hao wanao hamahama c usubiri ifike siku ya uchaguzi ndo uamue upande unaoutaka? siasa si kama nguo, ukiona mng'ao tu unakuvutia unanunua, TAKE CARE ALL OF U.

    ReplyDelete
  4. NILIPOSOMA SENTESI 'WIMBI KUBWA LA WASANII KUHAMA UKAWA KUHAMIA CCM' NIKAWA NA SHAUKU YA KULIJUA WIMBI HILO NI WANGAPI AROBAINI? AU HAMSINI?.AMA KWELI FEDHA FEDHEHA,WAANDISHI NJAA SASA HIVI MNANUNULIWA NA CCM KAMA VICHAA. MACHIZI KAZI KUBWA NI KUIREMBA CCM, NI KUIPA SIFA ZISIZOSTAHILI ZA KIHARAMIA,ZA UONGO,ZA KUJIMALIZA,ZA KIHUNI. NILIPOSOMA MAKALA HII []MPAKA MWISHO WA UANDISHI HUU NAWAKUTA NI WASANII WANNE TUU WANAOZUNGUMZIWA .LABDA NISEME KWAMBA MAJUKWAA YA UKAWA HAYANA MUSICIANS FIESTA KAMA INAVYOFANYA CCM ILI KUWAVUTA WATU.NI HADAA ZA KITOTO,KIHUNI.WENGI MNAOWAVUTA NI UKAWA DAMU ,WANAFUATA KUWAONA WASANII,KUUSIKILIZA MUZIKI WAO WA BURE [ WASANII HAWA WANALIPWA NA CCM KWA MABILLION WAPO KAZINI] KUTOKA PESA ZETU ZINAZOKOMBWA HAZINA NA BENKI KUU KWA AMRI YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA ] BAADA YA SHOW WANANCHI HAWA HAWAMSIKILIZI MAGUFULI WANATAWANYIKA.WAO NA LOWASSA,LOWASSA NA WAO,HAWADANGANYIKI.MAJUKWAA YA UKAWA KAZI NI MOJA TUU KUMWAGA SERA.LOWASSA PALE NI KIVUTIO CHA ASILI.UKAWA MSANII HALIPWI NI MWANACHAMA WA UKAWA SI MAMLUKI.KWA HALI HII HEBU WEWE WAWEKE KWENYE MIZANI MALAYA HAWA WANNE ROLE YAO KWENYE JUKWAA MAKINI LA SIASA UKAWA LINGEKUA NINI,NA NDIO KISA CHA KUKIMBIA HUKU WANALIA NJAA KALI UKAWA.PELEKENI VIGODORO HUKO HUKO CCM,WANAOVIHUSUDU BALAA,SODOMA NI HUKO CCM.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utayarudiarudia haya maandishi yako 25/10/2015

      Delete
  5. NA PIA NAJINDAA KUANDIKA KITABU' MALAYA KUJINGIZA KATIKA SIASA ZA KUISHABIKIA CCM,UCHAGUZI MKUU-2015. HII ITAKUA ZAWADI NA FUNDISHO KWA VIZAZI VIJAVYO

    ReplyDelete
  6. Njaa itawaponza
    CCM wengi wana ngoma huko
    Tutawazika kwenye mifuko ya Rambo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad