Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu, Fedrick Sumaye amesema kama Uchaguzi Mkuu wa Oktoba utakuwa huru na haki, basi umoja wa vyama vinavyounda Ukawa watashinda na kuingia madarakani.
Sumaye amesema ana uhakika kwa asilimia kubwa upinzani wana nafasi kubwa ya kushinda Katina uchaguzi mkuu ujao ni ndio sababu mojawapo iliyomfanya ajitoe CCM na kujiunga upinzani.
Akihojiwa katika kipindi cha Funguka kilichorushwa na kituo cha televisheni cha Azam Tv, Sumaye ambaye alikuwa waziri mkuu kwa miaka kumi katika serikali ya awamu ya tatu amesema amejitoa CCM kwa sababu ameona hali ndani ya chama hicho si nzuri na kuwa kuna nafasi kubwa ya upinzani kuingia madrakani.
Sumaye alisema hajajiunga na upinzani kwa kuahidiwa madaraka yoyote na kwamba lengo kubwa ni kutoa ushauri kwani anaamini ana uzoefu mkubwa wa kuitawala na atakuwa msaada kwao.
Akizungumzia kuhusu ufisadi ambapo awali alikaririwa akisema atatoka CCM endapo chama hicho kitamchagua fisadi, Sumaye alisema hana tatizo na Dk Magufuli lakini mfumo mzima wa chama na kuongeza kuwa hajawahi mahali popote kumtaja kwa jina Lowassa kuwa ni fisadi.
“Vita yangu ya ufisadi nimeanza maisha yangu yote na hakuna mahali popote nimewahi kumtaja Lowassa kuwa ni fisadi, taarifa ya Bunge haijawahi mtaja Lowassa kushiriki jinai yoyote katika suala la Richmond,” alisema Sumaye.
Kuhusu umiliki wa ardhi kubwa huku wananchi wengi wakilia hawana ardhi, Sumaye alisema haoni tatizo lolote kumiliki ardhi kihalali huku akisema eneo la hekari 300 analomiliki ni kidogo ikilinganishwa na vigogo wengine.
“Kama ukitupanga viongozi na kuangalia ukubwa wa mashamba tuliyonayo, mimi nitakuwa mkiani,” alisema Sumaye na kuongeza:
“Hivi kuwa na shamba ni dhambi? Nchi yeyote inayoendelea, watu ambao watabaki kwenye kilimo watakuwa na ardhi kubwa.”
Sumaye aliongeza kusema kuwa hata kama Ukawa hawataingia madarakani, hatarudi tena CCM na ataendeleza upinzani.
hatorudi ccm, hakuna anaemtaka na yeye analijua hilo, fix tuu
ReplyDeleteSumaye anawarubuni watz. anasahau alivyokuwa anamsema Lowasa, arudishe mashamba ya watu.
ReplyDeleteUNAFANYA KAZI KUBWA SANA MHESHIMIWA SUMAYE.UMEKUA WA MSAADA MKUBWA NA WA KIPEKEE KUITANGAZA UKAWA NA WANA MAGEUZI WOTE AMBAO HAWANA NAFASI YA KUPANDA MAJUKWAANI.SASA HIVI WEWE NI ADUI MKUBWA WA CCM.HILI TULILIJUA KWA SABABU HAWAKO TAYARI KUAMBIWA UKWELI KWAMBA KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO OCTOBA 25,2015 WATASHINDWA VIBAYA.HAWATAKI KUAMBIWA KUWA MAGUFULI NI FISADI MKUBWA AMEITIA HASARA SERIKALI MATRILLION YA PESA KWA KUSHINDWA KESI YA KUKAMATA MELI YA KIGENI ILIYOKUA INAVUA KIHALALI MAJI YA KIMATAIFA,TOZO LA MABILLION WANALOLIPWA BURE MAKANDARASI WANAYOIDAI SERIKALI MABILLION,UJENZI WA CHINI YA KIWANGO WA LAMI ZETU,WIZI MKUBWA TANROADS NA MIZANI,WIZI MKUBWA WIZARA YA UJENZI[RIPOTI YA CAG] KUWALIPISHA WAZABUNI MICHANGO YA MAGUFULI,KUNUNULIWA KIVUKO CHAKAVU MV BAGAMOYO AMBACHO HAKIJAWAHI KUFANYA KAZI HATA SIKU MOJA KWA BILLION 8.SASA BADO UNA HAMU YA KUMWITA MBADHIRIFI HUYO MWADILIFU?ACHENI MALIMWENGU CCM,MMEANGUKA,TENA VIBAYA. HONGERA SANA MHE.SUMAYE TUPO PAMOJA,TUTAKULINDA KIKAMILIFU.
ReplyDeletewee! nani ameanguka?? toa funza kichwani Anony 12.22 PM
ReplyDeleteLIAANZE KUANDALIWA SHITAKA LA UBADHIRIFU NA MATUMIZI HARAMU YA FEDHA ZA SERIKALI, PIA MATUMIZI MABAYA YA OFISI NA MADARAKA TRILLION NNE[4] SIJUI HILI NI SHAURI LA HAKIMU MKUU MKAZI WA KISUTU AU NI SHAURI LA UHUJUMU UCHUMI LINALOTAKIWA KUPELEKWA MAKAKAMA KUU MOJA KWA MOJA.HEBU TAMKA SAWASAWA, TRILLION NNE.TUNGEKUWA WAPI KIMAENDELEO?
ReplyDeletekondoo wasio kuwa na mkia oct tuna wasubiri ndo mtajua kama ccm imeanguka ama vip magufuri oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
ReplyDeletekaanguka mama yako msoga,mbebe umpeleke barazani kiotea cha nguruwe-mwitu wee.
ReplyDelete