Sumaye : Magufuli Amepoteza Dira......Sasa Anadandia Slogan za CHADEMA

Siku moja baada ya Dk John Magufuli kupachika jina lake kwenye operesheni ya Chadema ya M4C, Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye amemuelezea mgombea huyo urais wa CCM kuwa ni mtu anayedandia hoja baada ya kupoteza dira.

Wakati akipewa majibu hayo, DK Magufuli alikuwa akiendelea na kampeni mkoani Kigoma, ambako ajenda yake kuu ilikuwa ujenzi wa barabara, huku mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa akichanja mbuga mkoani Shinyanga.

Akiwa mkoani Kigoma jana, Dk Magufuli aliwaambia wananchi kuwa kirefu cha nembo ya M4C ni Magufuli for Change, badala ya Movement For Change, ambayo imekuwa ikitumiwa na Chadema kwa miaka takriban sita sasa, ikimaanisha “vuguvugu la mabadiliko”.

Dk Magufuli alisema yeye ndiyo mtu sahihi wa kuongoza mabadiliko na hivyo alama hiyo inatakiwa iwe na jina lake.

Lakini jana, Sumaye, ambaye ameingia Ukawa bila ya kujihusisha na chama chochote kati ya vinne vinavyounda umoja huo, jana alisema kauli hiyo ya Magufuli inaonyesha jinsi yeye na chama chake wanavyotapatapa.

“Ni aibu kubwa,” alisema Sumaye ambaye amekuwa mzungumzaji mkuu kwenye mikutano ya kampeni ya Lowassa.

“Yaani ni kama mtu anayezama baharini halafu maji yameanza kumuingia puani na kushindwa kupumua. CCM inazama na sasa inaanza kushika kila mahali kama mtu anayezama katika maji.”

Sumaye alisema hayo jana kabla ya Lowassa kupanda jukwaani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Malambo wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Akimchambua mgombea urais wa CCM, Sumaye alisema kauli yake imeonyesha jinsi asivyokuwa na aibu na imedhihirisha jinsi alivyopoteza dira kwa kudandia hoja na mipango ya wapinzani.

“Sisi tunadai mabadiliko na kama na dawa ya kunguni ni kukitoa kitanda na kukitupa nje wakaozee huko,” alisema Sumaye huku akishangiliwa na wananchi.

Kwenye mkutano huo, Lowassa aliyepokewa na maelfu ya wananchi waliokuwa wakimsubiri, aliahidi kumaliza kero ya maji kwenye wilaya kwa kuendeleza mradi wa kutumia maji ya Ziwa Victoria lililopo umbali wa kilomita 30.

Mbunge huyo wa zamani wa Monduli alifika eneo hilo saa 10:00 jioni na kukimbiliwa na wananchi waliotaka kumshika na kusababisha polisi kutumia nguvu ya ziada kuwazuia.

 Akizungumza na wananchi wa Bariadi, Lowassa alirudia tena ahadi yake ya elimu ya bure akisema kuanzia Januari mwakani hakuna mwanafunzi atakayelipa ada kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu.

Pia aliahidi kuboresha kilimo ili kiwe cha kisasa na cha kibiashara, huku akisisitiza msimamo wake kuwa Serikali yake haitamvumilia mtu atakayeshindwa kwenda na kasi yake.

Mgombea huyo pia alifanya mikutano mingine Maswa na Busega.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sumaye rudisha mashamba ya watu kwanza. huoni aibu??

    ReplyDelete
  2. kuwa na mshipa wa aibu sumaye miaka kumi hujaridhika na madaraka uchu wa madaraka umekupotezea dira wewe ndo fisadi wa kutupa muache magufuli wetu sisis anatosha umeula wachuya sasa wewe huoni au umekua kipofu ulivoenda chadema muogope mungu rudisha mashamba ya wananchi unaongea madudu tunakuangalia2 magufuli mpaka ikulu naitaeleweka2 unaongea kama umeazima ufahamu kwa mtu kumbe wa kwako

    ReplyDelete
  3. Simawe hana lake kazi yake muhimu nikuchambua wanayoyasema CCM hana mpya bepari anachofanya ni kupinga nguvu za kifyagio cha mafisadi pamoja na kukombolewa kwa mashamba waliyojimilikisha wakiwa CCM

    ReplyDelete
  4. Yaani nyie udaku ni maGenius yaani Tz tuna watu wenye akili kupindukia badala yake ni bora mgepewa nafasi maalumu ktk mambo ya ubunifu leo tz tungetengeneza nyukilia ya nishati wenyewe pasipo kununua vipuri nje maana habari mnanavyo zitengeneza utafikiri watz wote ubongo zero nyinyi ndio kila kitu

    ReplyDelete
  5. Wataiba na kujeza sana
    Lakini wetu Lowassa

    ReplyDelete
  6. Na nyie rudisheni twiga wetu mliopandisha ndege na yeye atarudisha mashamba

    ReplyDelete
  7. Sema Sumaye wapashe ni Nani Tanzania waziri mkuu aliyekaa miaka kumi
    Unaijuwa Siri zote za CCM na serikali
    25 October mwisho wao

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad