TAMKO LA TAASISI YA KIISLAMU YA IMAM BUKHARY JUU KAULI ZA NDUGU EDWARD LOWASSA NA ASKOFU GWAJIMA WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA
Ndugu Wanahabari,
Assalaam Alaykum,
Hivi karibuni Taifa letu limetikiswa na maneno ya hatari yaliyotoka katika vinywa vya watu wawili mashuhuri hapa nchini. Maneno ambayo endapo yatapuuzwa yatasababisha mpasuko mkubwa wa kijamii na pengine maafa, na hatimaye kubomoa misingi imara ya taifa iliyojengwa na waasisi wa Taifa hili. kauli hizo ni zile zilizotolewa na mgombea urais wa CHADEMA Ndugu Edward Lowassa na kiongozi wa Kanisa la ufufuo na uzima, Askofu Josephat Gwajima.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Ndugu Edward Lowassa amenukuliwa akiwa Kanisani Mkoani Tabora akiwaomba Waumini wenzake wa Madhehebu ya Kilutheri kumuombea sana awe Rais wa Taifa letu kwa hoja kuwa nchi hii haijawahi kupata Rais Mlutheri.
Naye Askofu Josephat Gwajima ambaye ni mshirika wa karibu wa Lowassa amenukuliwa pia akielezea ndoto yake ambayo bado haijatimia ya Kuiona Misikiti ya Tanzania ikigeuzwa kuwa “Sunday Schools” za watoto, pamoja na Masheikh na Maimamu kukimbizana kwenda mbele ya msalaba wa Bwana Yesu Kristo (AS).
Maneno haya ya Ndugu Lowassa na yale ya Askofu Gwajima yakitazamwa kwa idadi ni machache sana, lakini kwa uzito wake ni mabaya tena yenye hatari kubwa kwa umoja wetu wa kitaifa.
Maneno hayo yanaweza kulisambaratisha taifa kwa vile yanaonyesha dhamira mbaya waliyo nayo viongozi hao katika kuibomoa misingi ya Utaifa ya umoja na mshikamano, na badala yake kujenga misingi ya udini katika siasa na utawala.
Kadhalika matamshi hayo yanaonyesha dhamira yao ovu ya kujenga utawala wenye kufuata misingi ya ubaguzi wa kidini endapo watafanikiwa kushika uongozi wa nchi, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa Uislamu unafutika kabisa katika nchi hii.
Ndugu Wanahabari, tujikumbushe kwamba Edward Lowassa anaomba awe Rais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mchakato wa kumfikisha huko umeratibiwa na Askofu Gwajima. Kila mmoja kati yao ameweka wazi dhamiri yake.
Wakati Ndugu Lowassa amejikita katika fikra za kupandikiza dhana ya ubaguzi wa kidini kuwa kigezo cha kuchaguliwa katika uongozi wa nchi, mwenzake Askofu Gwajima anatabiri kuwa mara tu baada ya kufanikiwa kushika hatamu za utawala, kitu cha kwanza kitakachotokea ni Misikiti kugeuka kuwa vituo vya kuwafundishia watoto imani ya Kikristo na Masheikh wote watapanga mistari kwenda kubatizwa kuwa Wakristo. Kwa maana nyingine Uislamu utafutika kabisa hapa nchini katika utawala wa Lowassa.
Ndugu wanahabari, Ushirikiano na ukaribu wa Lowassa na Askofu Gwajima si wa kuutazama kwa jicho moja tu. Tukumbuke kwamba ni Askofu Gwajima huyu huyu aliyekerwa kwa kuona Sehemu ya kuswalia Waislamu katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akieleza porojo zake za dhamira ya kujengwa Msikiti katika ofisi za Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG.
Ni Askofu Gwajima huyu huyu aliyekerwa na mchakato wa Mahakama ya Kadhi hadi akalazimika kutoa lugha zisizo na staha kwa watu wazima wakiwemo viongozi wakuu wa kidini hapa nchini.
kwa upande wake ndugu Lowassa huyu ndiye aliyefanikisha mkataba kati ya Serikali na Makanisa (MoU), mkataba ambao Waislamu tunaulalamikia mpaka leo hii.
Wanaposhirikiana wawili hawa pamoja na historia ya matukio yao hayo ya ‘KIBAGUZI’ kisha kila mmoja akatamka bayana maneno yanayotikisa misingi ya Utanzania na kuweka mbele ajenda zao za udini, si busara kuwanyamazia kwa maslahi ya Umoja wetu wa Kitaifa.
Haiwezi kuwa busara kwa Jamii ya Waislamu na watanzania wanaopenda amani, kukaa kimya wakati viongozi wa kisiasa na kidini kama walivyo Askofu Gwajima na Ndugu Lowassa wanatangaza hadharani nia yao ya kuivunja misingi ya utaifa na pia kukamia kuifuta dini yetu hapa nchini na kuwabatiza Masheikh nchi nzima, na kisha baada ya hapo kuigeuza Misikiti kuwa Sunday Schools za watoto wa kikristo. Hii ni dharau iliyochupa mpaka kwa dini tukufu ya Kiislamu na kwa waislamu wenyewe.
Ndugu Wanahabari, Taasisi yetu ya "Imam Bukhary Islamic Foundation" imekaa kimya kwa muda mrefu ikitafakari matukio hayo mawili ili kuona ni hatua gani stahiki zitachukuliwa kutokana na “cheche” hii ya moto wa hatari wa ubaguzi. Mwishowe tumeona tutahadharishe na kuwakumbusha Waislamu pamoja na Watanzania kwa ujumla yafuatayo:
(1) Kwa sauti ya juu Watanzania wote tumkemee na kumpinga Ndugu Edward Lowassa katika mpango wake wa kuona urais wa Tanzania unastahiki kwa zamu za Madhehebu ya dini, na tumwambie asiwagawe Watanzania kwa misingi ya kiimani
(2) Tuwakumbushe Ndugu Lowassa na Ndugu Gwajima kwamba Waislamu kamwe hawajasahau namna mchakato wa Mahakama ya Kadhi ulivyovurugwa kwa kuwatumia maswahiba wao, ambao leo hii wamejidhihirisha kuwa pamoja kwenye kambi zao za kampeni katika kuutafuta huo urais wa Tanzania, kwa dhana mbaya eti lau mchakato ule ungefanikiwa basi ungembeba mmoja kati ya wagombea wa urais.
(3) Tamko la Gwajima kuwa katika utawala ujao misikiti itageuzwa kuwa Sunday Schools za Watoto na Masheikh watakwenda kubatizwa na hivyo Uislamu kufutika hapa nchini, si tu kwamba ni maneno ya uchochezi, chuki na dharau kwa Waislamu, bali pia ni kipimo tosha kwa watanzania wote kutambua kuwa kundi hili halifai kiuongozi na ni wajibu wa kila mtanzania kumhadharisha mwenzake juu ya kumpigia kura Ndugu Lowassa na kundi lake.
(4) Kila Mtanzania anapaswa kufahamu kuwa, kumpigia kura Lowassa ni hatua moja katika kuvunja misingi ya amani na utangamano wa nchi yetu, kutokana na dhamira yake ya kuutazama uongozi wa nchi katika sura ya udini na umadhehebu. Lakini pia kila Mwislamu atambue kuwa kumpigia kura Lowassa itakuwa ni kuutimiliza utabiri wa Askofu
Gwajima wa kuwabatiza Masheikh wote Tanzania na kuigeuza Misikiti kuwa Sunday Schools kwa watoto wa kikristo.
Ni vizuri sisi Waislamu ambao ni waathirika wa mbinu chafu iliyotumika kuikwamisha Mahakama ya Kadhi, tumuulize Ndugu Lowassa: ameahidi kutatua kero kadhaa akiingia Ikulu, lakini kwanini hajapatapo kuitaja Mahakama ya Kadhi? Je, Lowassa hujui kuwa kutokuwepo kwa Mahakama ya Kadhi ni kero kwa Waislamu?
(5) Tuendelee kuhubiriana udugu wetu wa kitanzania na wale wote wenye nia mbaya tuwakemee na tuwazuwie kufikia kilele cha madaraka kitakachowawezesha kutimiza dhamira zao bila woga ili amani yetu idumu.
(6) Taasisi inajipanga kuandaa Semina maalum kwa Maimamu na baadhi ya Masheikh ili kujadili njia iliyo bora zaidi ya kujikinga na njama za wale wote ambao wanataka kulipasua Taifa letu kwa maslahi yao binafsi, wasifikie kwenye malengo yao hayo maovu.
Na tunawaomba Masheikh na Maimamu wa Misikiti yote Tanzania pamoja na Waislamu wote kushiriki kuwazindua Waumini kila pahala kote nchini kuwazindua Wananchi kwa ujumla juu ya hatari ya kuwaweka juu ya uongozi wa nchi yetu watu wenye dhamira ya kujenga dhambi ya ubaguzi wa kidini ambayo ni kansa itakayokula mwili wa Taifa na hatimaye kuliangamiza kabisa.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Sheikh Khalifa Khamis
MWENYEKITI,
TAASISI YA KIISLAMU YA IMAM BUKHARY
(IMAM BUKHARY ISLAMIC FOUNDATION)
24/09/2015
Tumejua mbinu zao waislamu tushikamane
ReplyDeleteNI SHIIDA
DeleteCCM Bao la kona
ReplyDeleteMtatumiwa kila kona mashehe wenzenu wanasota lupango
CCM hiyo
ulisahau kusema ccm oyeee.wewe unatumiwa kama wewe na hao madhalimu ccm,sisi waislam hatukukutuma.sasa unasemaje.unataka nini,unamsemea nani. ,ulikua wapi kugombea udiwani wa ccm.kwa kununuliwa kwako na january makamba unapoteza sifa zako za utu na heshma ya waislam wote wapenda mageuzi na maendeleo.nani akuunge mkono muhuni tuu wa mtaani wewe.chini ya serikali dhalimu ya ccm waislam tumenyanyasika sana kwa miaka 55.tumeuawa,tumepigwa,tumefungwa,tumewekwa na tunaendelea kuwekwa vizuizini bila sababu,kinyume cha sheria za nchi na za kimataifa,we unaona sawa tuu.baradhul hayawan..kwa taarifa yako ccm inangoka octoba 25.kamwambie maneno haya ridhwan na baba yake waliokutuma na ukakubali kuuza utu wako.
ReplyDeleteHii siyo ishu ya waislamu peke yao. Ni kwa Wa Tanzania wote kwa pamoja kuungana na kupinga ubaguzi wa dini, kabila.. Waislam naWakristo kuungana kuwapiga vita hao kina Gwajima nakundi lake, ikiwezekana kuchoma moto kanisa lake, endapo selikari haitomchukulia hatua za kisheria. Mimi kama Mkristo roho inauma sana kuona huyu Gwajima bado anaishi mitaani mpaka leo
ReplyDeleteTUNAKUJUA VIZURI SANA WEWE SHAYKH KHALIFA HAMISI,ULIWAHI KUA IMAM WA MSIKITI WA MTORO,NI MPUUZI.UNAKUMBUKA ULIFUKUZWAJE MSIKITI WA MTORO? TUNAKUULIZA. TUNATOBOA WEWE ULIANZA KUUNDA MAGENGE YA WAHUNI KUUDHALILISHA UISLAM NA ULIPOGUNDULIKA MWENYEKITI WA WADHAMINI WA MSIKITI SHAYKH SAID SALUM BAKHRESSA AKIAMBATANA NA VIONGOZI WENGINE WA MSIKITI WAKAKUONDOA KWA KUKUFUKUZA KWA NGUVU,FEDHEHA NA MAKOFI MENGI TUU.JEE HUKUKIMBILIA POLISI KUCHUKUA RB? TUNAKUULIZA. TUNAKUJUA NI WEWE YULE WA JANA,WA LEO NA WA KESHO.UMEJAA NA UMEJAALIWA HADAA.PANDA MAJUKWAA YA CCM,UFE NAO.HADANGANYIKI MTU HAPA.
ReplyDeleteKapigeni kura kila mtu anampenda mtu wake kwa sababu zake wee kama team lowasa kimpango wako na mwingine kama team makufuli kimango wake mwishobwa siku kila mtu anakula kwa urefu wa kama yake kama mbuzi ila mabadiliko sahau nani ataenda kijijini kwenu ampe babu yako au bibi yako trekta alimie kutoa umaskini,,,,hujiulizi ,,,,,,,,,Sidanganyikiiiii kura yangu nampa ni mtakae.
ReplyDeleteHUU WARAKA COPYRIGHT MUUNDO WA CCM.NI AINA YA UANDISHI YA JANUARY MAKAMBA,TUNASEMA KWA KUSISITIZA NI BARUA ILIYOANDALIWA, KUHAKIKIWA NA CCM KAIANDIKA JANUAKY MAKAMBA,KHALIFA AMEKABIDHIWA TUU KUISAINI, KUIWAKILISHA KWENYE VYOMBO VYA HABARI HUKU AKIPEWA BAHASHA LA FEDHA CHAFU, HARAMU ZA CCM,YALE YALE YA DR SLAA;YA MTIKILA, YA LIPUMBA,YA AIDAN WA TWAWEZA.AMA KWELI UANAHARAMU WA CCM UMEWAHARAMISHA TAMAA KUL HAWA,WAMEJIVUA NGUO MBELE YA JAMII WAPO UCHI WA KIMA NA NGEDERE .UPENDE USIPENDE,ULIE UCHEKE RAIS WETU WA AWAMU YA TANO NI MUHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA.HALAFU,KWA MIAKA KUMI UTAKAA NA KUDUWAA NA KUJUTIA KWANI UTAKUA UMEMSALITI MAPEMA RAFIKI WA DHATI WA WAHITAJI WOOOOOTE.TUTAKUA TUNAKUAGALIA TUU UNAVYOSOTA.
ReplyDeleteKaka umenifanya nisitoe koment yangu coz ndo exactly nilichotaka
DeleteKusema.
KAZI YA MAKAMBA
Akili ni mali kila mtu ana zake. Nyinyi watu mnaakili vipi. Ujinga mnaoutoa inaonekana wazi hamna elimu. Umaskini na Ujinga wa mwafrika unaletwa na Waafrika wajinga kama hawa. Elimu hawana wanachobaki kukifanya ni kutumimka na wanasiasa badala ya kujikwamua kielimu. Kama wewe ni mzanzibari kwa maneno kama haya nakuonea huruma kamwe Zanzibari hataendelea. Nimewaona Wazanzibari wakitaka maendeleo na kuchoshwa na CCM. sijui vitisho hivi umevitoa wapi. Adui mkuu wa maendeleo ni ujinga na upumbavu. Ndio huu.
ReplyDeleteAcheni kuwadanganya watanzania wa jamii ya kiislaamu.Kunamatatizo mengi yanawakabili waislamu hmuzungumzii wala kuyafanyia kazi.Ukosefu wawalimu wa kiislamu kufundisha shule za msingi,maimamu waliofungwa jela Zanzibar bila kufunguliwa kesi yoyote,Shule za kiislamu zimekuwa za mwisho kwenye matokeo hamuoni.Chakushangaza CCM wanaposema kuwa hawakotayari kuiachia ikulu kwa gharama zozote zile sio uvunjifu wa amani.Mbona hayo hamuyaoni.Taasi ya imamu bohary sio jumuiya ya waislamu wote.Mnaonesha ubinafsi ,kuhingwa,na mmejaa fitna.Hamtuibadilishi tena.Hatudanganyingi.Mbona hamkubiga kelele wakati serikali ilipokataa mswada ma mahakama ya kadhi isijadiliwe bungeni baada ya baraza la maaskofu tanzania kupinga.Mlifunga mdomo.leo ndio mnazungumzia hilo.Hatudanganyiki.Tutampigia kura Lowassa
ReplyDeleteManeno ya gwajima na lowasa labda kama mseme si kweli kama ni ya kweli akili ku mkichwa.hayafai kusemwa na viongozi wa dini au wa chama.mpunguze mahaba use ur head.
ReplyDeleteSisi wenye uchungu na dini yetu tukufu, TUMEKUELEW na TUTAYAFANYIA KAZI.
ReplyDeleteJamani kikwete makamba magufuli na ccm kwa ujumla mmefikia pabaya sana kweli mnataka kuingiza nchi pabaya kisa mpate kula mnasikitisha sana..sasahv mnashindana na Mungu mwenyewe wala sio watanzania na Mungu atawaumbua vibaya sana
ReplyDeleteSISIEM ACHENI HIZO, MBONA MNATAPATAPA??????????
ReplyDeleteza siku ustaadh khalifa hamisi,umeanza tena unafiki wako.safari hii ukiwa kada ccm.siku unapigwa pale msikiti wa kwa mtoro nilikuwepo.wallah kama siyo kufukua mbio kama za mshindano na kukimbilia kituo kikuu cha polisi msimbazi ukaokolewa sijui siku hiyo ingekuwaje wangekufanya vibaya .usiwadanganye watu kaka tanzania ya watanzania wa leo haidanganyiki,tumeshachoka na ccm haturudi nyuma mtanzania,amekwishaamua kuipiga chini ccm octoba 2015.usisumbuke na hadaa.kama ni kuganga njaa haya,lakini usitulaghai utampata nani mrundi wewe.
ReplyDeleteSisi waislam inatakiwa tuchambue kwan sio kila kiongoz anafaa kupewa urais wengine ni nyoka sio wazuri
ReplyDeleteHApo wote mliotengeneza majina ili muonekane ni waislamu siyo waislamu tunajuwa .waliosema hao mashehe ni cha ukweli .mbona hatujasikia tamko la waislamu sikuzote tunasikia matamko ya viongozi wa kikristo .wamesema ukweli viongozi wa dini wakae pembeni wawaachie wana siasa .nyinyi acheni ujinga.lowassa anashabikia udini halafu nyinyi mnasema mashehe wametumwa .subirini muone impact ya tarehe 25
ReplyDeleteKamwe tusitumie dini kwa dhamira ovu Mungu ni Mkubwa sana anaona mpaka yaliyomo katika nafsi zetu! Tusijisahau sana hapa duniani tunapita tu usipoadhibiwa hapa duniani kumbuka kuna siku ya hukumu utaweza kuhimili malipo ya madhambi yako? Tukumbuke kila wakati kuwa Mungu yupo na anaona kila kinachoendelea, TUSIJISAHAU! Tumuombe Mungu atuvushe salama katika kipindi hichi cha mpito!
ReplyDeleteasante januari makamba,tusubiri octoba 25.na,sikiliza kwa uhalifu huu jiandae kusota lupango,tena basi kwa kuwa nyinyi ccm mnatamba kwa kutumia zile sheria kandamizi za kuwaweka watu kizuizini kwa kisingizio cha usalama wa nchi,kitakachofanyika ni kuitumia sheriazile zile zile kwenu wewe na kwa baba yako yusuph makamba.mahakamani mtapelekwa kwa sababu mashtaka yenu ni mengi,mkiwekewa dhamana mtakimbia nchi.hakuna dhamana.
ReplyDelete