Kituo cha Televisheni cha StarTV ni kati ya vituo vikubwa vya habari hapa nchini kilichowahi kupata heshima ya kipekee kwa habari zake zilizokuwa hazina upendeleo.
Hata hivyo tangia kuanza kwa harakati za kampeni wiki mbili zilizopita kituo cha StarTV kimekuwa kimekuwa kikirusha matangazo yanayoonyesha ubaguzi na chuki kwa mgombea Urais kupitia UKAWA Edward Lowassa.
Tangazo la hivi karibuni linalorushwa na kituo hicho mpaka sasa ni lile linalochochoea udini likimhusisha Edward Lowassa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Watu kadhaa waliohojiwa kuhusiana na matangazo ya kituo hicho yanayokuwa ni maalum kumdhalilisha mgombea Urais wa UKAWA Edward Lowassa wamesema kituo hicho cha StarTV kimepoteza uhalali wa kuwa chombo cha habari.
Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa Peter Kuga Mziray ameshangazwa na TCRA na Tume ya taifa ya uchaguzi NEC kunyamaza kimya bila kukemea upuuzi unaofanywa na kituo hicho.
Naye mhadhiri wa chuo kikuu Professa Gaudence Mpangala amesema mauaji ya halaiki Rwanda yalisababishwa na chombo cha habari kufanya uchochezi wa kuwagawa watu kama wanavyofanya StarTV.Amesema ni kitendo cha aibu chombo cha habari kinachojiita kinajitegemea kuegemea upande mmoja hadi kufikia kuandaa matangazo ya kukashifu mgombea wa urais anayeonekana tishio kubwa kwa watawala.
Mwananchi mmoja kutoka Mwanza aliyejitambulisha kwa jina la Said Yusuph alisema itafika mahali vijana wafuasi wa UKAWA Mwanza wataishiwa uvumilivu na wanaweza hata kuvamia kituo hicho kutokana na vitendo visivyo na maadili vya kumkashifu mgombea wa UKAWA Edward Lowassa.
Kituo cha StarTV kinamilikiwa na Anthony Diallo ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza.
Televisheni ya Star TV yatuhumiwa kuchochea vurugu kwa kumkashifu Edward Lowassa
September 12, 2015
Tags