Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yaingilia Kati Ugomvi wa UKAWA na CCM Uliosaabisha Mauaji

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema imepokea kwa masikitiko taarifa za kutokea kwa mauaji katika Kijiji cha Mangucha, Wilaya ya Tarime wakati wa kampeni za uchaguzi ambapo mkazi wa kijiji hicho,

Mwita Waitegi aliuawa na imelaaani vikali mauaji hayo pamoja na kuwahimiza viongozi wa vyama vya siasa kuwa makini na wananchi wanawaongoza
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na kusainiwa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, inasema tume inakemea vikali na kwa nguvu zote ukiukwaji wa maadili unaosababisha uvunjifu wa amani na kusababisha vurugu.

“Kwa mujibu wa taarifa zilizopokelewa na tume, pamoja na mambo mengine, kwa kiwango kikubwa kifo kilisababishwa na fujo, vurugu na purukushani kati ya wafuasi wa vyama vya CCM na Chadema. Vurugu na fujo hizo ni kinyume kabisa cha maadili ya uchaguzi ya 2015 yaliyotiwa saini na vyama vyote vya siasa,” inasema taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo inasema maadili ya uchaguzi yanazuia mtu yeyote kuwa au kubeba silaha yoyote ikiwa ni pamoja na silaha za jadi au zana yoyote inayoweza kumdhuru mtu katika mkutano wa Kampeni au mkusanyiko wowote wa kisiasa.

“Kutokana na kutozingatiwa kwa Maadili ya Uchaguzi, 2015 kifo kimetokea na baadhi ya wananchi, wanachama wa vyama hivi vya siasa kuumia, tume kwa mara nyingine imekumbusha na kusisitiza vyama vyote vya siasa na wanachama wao kuzingatia Maadili ya Uchaguzi ya 2015.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad