Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imepuuza malalamiko ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) juu ya kauli ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Abdallah Bulembo, kuwa chama chake hakitakuwa tayari kuiachia Ikulu kwa namna yoyote ile, ikisema ni ya kisiasa na hayana madhara yoyote.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, amesema kwa sasa kila chama kipo kwenye kampeni za kutafuta ushindi, hivyo kauli kama hiyo inaweza kutolewa na upande wowote ikiwa ni mbinu ya kujipatia ushindi.
“Ingekuwa kauli yake tafsiri yake ni kuwa hawatakubali matokeo ya uchaguzi hapo tume ingekuwa imehusika na ingezungumza kwa kuwa tulishasema kila chama shindani katika uchaguzi huu kinatakiwa kukubali matokeo yatakayotangazwa na tume,” alisema.
Alisema hadi sasa NEC haijaona cha kujibu juu ya kauli hiyo na inaichukulia ni matamshi ya kisiasa ya kampeni.
Hivi Karibuni Bulembo akiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Kigoma, alidaiwa kutoa kauli kuwa chama chake hakitakuwa tayari kuiachia Ikulu kwa namna yoyote ile.
Mwenyekiti wa Ukawa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akizungumza na waandishi wa habari, juzi alilalamikia kauli hiyo na kuitaka NEC kulaani kauli hiyo kwa kuwa uchaguzi ni ushindani na hakuna mwenye maamuzi zaidi ya wapiga kura.
Mboe tulia mbona ikulu yenu
ReplyDeletetulikwisha sema mara nyingi kwamba hatuna imani na tume ya taifa ya uchaguzi.hapa tufafanue siyo tume yote[in entity] hapana.wapo watumishi waaminifu,wakweli na wanaofanya kazi zao vizuri ndani ya tume lakini hawana maamuzi ya mwisho.huyu mwenyekiti wa tume jaji mstaafu damian lubuva ndiye kila kitu kwenye tume,ndiye msemaji mkuu,ndiye mpindishaji mkuu,ndiye mtetezi mkubwa wa ccm,ndiye kinara wa mbinu mkakati za matamko machafu na ya vitisho vya ccm dhidi ya watanzania walio wengi.huyu ni jaji mstaafu damian lubuva mwanachama hai wa ccm anayeukandamiza ukweli na kupuuzia hatari halisi.matamko hatari ya abdallah bulembo kwamba ccm itajichimbia ikulu hata kama ikishindwa kwenye uchaguzi mkuu yalipaswa sio tuu kuyakemea bali pia kumfungia bulembo kupanda jukwaa la kampeni na siasa angalau kwa miaka kumi.huyu anatangaza kuiasi katiba lubuva anacheka tuu'aah hayo ni maneno ya wana siasa'mwisho wa siku 'aah nilidhani ni utani kumbe kweli'.yote kwa yote sisi wananchi wa tanzania tulio wengi tayari tulikwisha amua,kuyaleta na kuyapokea mabadiriko.kamwe hatutazuiwa na wahalifu wachache.kwa amani na utulivu tutapiga kura zetu october 25,2015,kwa amani na utulivu tutashangilia ushindi wa MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA rais mpya wa awamu ya tano KWA WIKI NZIMA -SIKU SABA -kuanzia tarehe 26 octoba 2015 hadi tarehe 1 november 2015.hapo tutaimba,tutacheza,tutakunywaTUTAKULA,vimbwanga,vituko kede kede,tutatamba wa bunju atakaribishwa kibamba,wa kigamboni gongo la mboto wa rukwa tanga wa mbeya mwanza,yaani wee acha tuu.HII NDIYO TANZANIA MPYA YA LOWASSA INAYOKUJA.
ReplyDelete