Ujue Ukweli wa Edward Lowassa Kukimbia Midahalo ya Urais

Lowassa na Magufuli
Vyama vyote vya siasa vimekubali kufanya mdahalo wa wagombea wa Urais kwenye vyombo vya habari lakini vyama vinavyounda UKAWA vimekataa kushiriki kwenye midahalo hiyo kwa kutoa sharti moja la kutomshirikisha mgombea wao na badala yake waende wenyeviti wa vyama.

Utaratibu wa dunia nzima kwenye midahalo wanahudhuria wagombea na siyo wenye viti wa vyama... Yaani Rais Kikwete aache majukumu yake ikulu halafu aende kwenye vyombo vya habari kufanya midahalo wakati kwenye midahalo wanazungumzia sera za chama husika na sasa aliyebeba sera za CCM ni Ndugu Magufuli.

Baada ya kufanya uchunguzi sababu zifuatazo zimebainika kuwa ndiyo vigezo vya kumfanya mgombea wa UKAWA ndugu Lowassa kususia midahalo hiyo
1. Afya yake ni dhaifu na haimruhusu kukaa muda mrefu bila kupewa dawa ya kumuongezea nguvu. kwenye mikutano yake ya kampeni hajawahi kuzungumza zaidi ya dakika 15, sasa atawezaje kuhudhuria mdahalo akaongea zaidi ya nusu saa?

2. Amehusika sana kwenye kashfa nyingi za ubadhilifu wa mali za umma na hana uwezo wa kukataa ukweli huo, hata alipoulizwa na waandishi wa habari huko Dodoma alikataa kulijibu hilo swali, na endapo atahudhuria kwenye mdahalo wowote hilo swali hawezi kuliepuka

3. Chama chake hakina sera nzuri, anakosa kitu cha kuongea awapo mbele ya watu kwakua chama chake hakijaandaa ilani nzuri yenye sera za kumkomboa Mtanzania. Wakati wenzake wanatoa sera za kupunguza gharama za ujenzi yeye anamwaga sera za kuwatoa jela akina Babu Seya na kubomoa nyumba za nyasi nchi nzima kwa muda wa siku 100

By Aisha Idd
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. AKILI KICHWANI WATANZANIA,
    MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  2. eeeh mungu wangu,mungu wangu watu wazima wanafyatuka.ama kweli kutumwa kwa njaa ni matatizo.ni hivi.tangu uanze mfumo wa vyama vingi ni mgombea yupi wa urais wa ccm aliyewahi kushiriki mdahalo wa wagombea urais.anzia MKAPA MIAKA 10 NJOO KIKWETE MIAKA 10.muache mwinyi.Hivi ni kwa nini mnakuwa waongo,wanafiki,wenye hoja finyu zisizo na mashiko.Miaka 20 CCM walibembelezwa kwa kiila hali na kupigiwa magoti hawakujitokeza tena kibaya zaidi bila hata kutanguliza sababu,narudia MIAK 20 YA MKAPA NA KIKWETE MLIFUNGA MILANGO YA MIDAHALO YA WAGOMBEA WENU,leo hii ccm mnasema mmezinduka mnamtaka MHESHIMIWA LOWASSA.Mmeota nini ccm mnaongelea kuikumbuka shuka wakati umekwisha kucha?MNAZO SIKU 46 HIVI ZA`UNAFIKI WENU TUMEKWISHA GUNDUA TENA MNAOOMBA NI NYINYI CCM NA SIO TAASISI HURU-KWENDENI ZENU.TUMEKWISHA AMUA LOWASSA IKULU KIAPO-HATUTOBADIRIKA KATU.Mmekwisha ccm mmekwisha mnaondoka.TUNA IMANI NA LOWASSA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao wote ulowataja ambao hawakushiriki midahalo ni CCM, hata kama Magufuli angekataa mdahalo tusingeshangaa kwakuwa ni CCM ni kawaida yao kutoshiriki midahalo. Huyo 'fisadi papa' kwa sasa sio CCM, na mlisema akija huko atafuata 'mfumo' wenu.....kulikoni hataki mdahalo?? Au nayeye ni CCM?? Mtajutraaaaaaaaaa

      Delete
    2. Habari za asubuhi, uko pouwa weye? Inaelekea ulikuwa umelala, umekurupuka nakuanza kucomment. Hebu kanawe kwanza, kisha waulize waloamka mapema hii mada imeanzia wapi....maana wala hujui 'mtu wenu' Mbatia alizungumza nini na wanahabari.........WAKUKURUPUKA MUPOOOOO

      Delete
  3. Kama kuongea hawezi anaweza vitendo, angefanya vitendo hivyo tangu alivyokuwa madarakani tena ngazi ya juu kabisa. Hakuna jipya hapo. Mkubali tu hawezi kuongea muda mrefu kwa ajili ya afya yake.CCM OYEEEEEEEE

    ReplyDelete
  4. Ukawa mtaelewa tuu

    ReplyDelete
  5. Afadhali wadau hapo juu mmempa vyake man's ningemtukuna kweli mshenzi uyo kwani ccm imetufanyia nini NASA Nazi kupiga madomo tuu na mauwongo

    ReplyDelete
  6. Hizo polojo mtoa mada anazozileta hapa ndo zilizotufikisha hapa tulipo hoi bin taabani. Vitendo vyenye ukweli na vinavyotekelezeka ndo tunavyohitaji na si kufanya comparison za ajabu ajabu hapa.

    ReplyDelete
  7. Unajua uliyepost hiyo mada Una shida hizi propaganda za zamani siyo leo,unaweza ukaongea masaa matano lakini pumba tu

    ReplyDelete
  8. Hivi ataongea nini kwamfano?? Kabla hajatoka CCM pale aliposema asomtaka CCM atoke yeye, alihojiwa na waandishi wa habari akasema swali nikilipenda nitajibu, nisilolipenda sijibu, sasa hapo kwenye mdahalo hakuna muda wa kuchagua maswali, unatakiwa uyajibu yote, ATAWEZA????

    ReplyDelete
  9. NI HIVI NAOMBA UKAWA KWENYE MDAHALO KAMA UTAKUWEPO,UKAWA IWAKILISHWE NA HIZA TAMBWE.UKAWA TUNAMWAMINI NA ATAMTOA NISHAI MAGUFULI KWA SABABU ANA TAKWIMU ZA WIZI MKUBWA NA UDHAIFU WA MAGUFULI .SASA HIVI MHESHIMIWA LOWASSA KESHA ANZA REHERSAL YA KUAPISHWA KUCHUKUA DOLA.MHESHIMIWA KWA WAKATI HUU HANA NAFASI HATA KIDOGO YA KUIONA SURA YA MAGUFULI ANAPOKEA MAELFU YA VILIO NA MANUNGUNIKO HALALI YA WATANZANIA NCHI NZIMA YAANI HANA HATA DAKIKA YA KUPOTEZA BURE.WAKATI WAKE WA KUPUMZIKA ANALO LILE BUKU LA BAJETI YA SERIKALI 2015/2016 AMBALO NDANI LIMEJAA MATUMIZI MABAYA ASILIMIA 40.LINAFANYIWA KAZI USIKU NA MCHANA KWA SABABU HAZINA IMEKAUSHWA NA CCM,NA MHESHIMIWA LOWASSA ATAANZIA UTAWALA WAKE NA TREASURY NYEUPEEE.HAKUNA HILA YA CCM INAYOKOSA JIBU,TENA LAPAPO KWA PAPO.

    ReplyDelete
  10. ZAIDI YA MARA 20 MAGUFULI AMEKUA AKIKIMBIA WAANDISHI WA HABARI MSEMO WAKE MAARUFU WA 'NO COMMENT' USISHANGAE WEWE JUHA WA CCM KAMA KWENYE MDAHALO UWE WOWOTE ULE ATAENDELEZA LIBENEKE LA MAJIBU YAKE YA SIKU ZOTE 'NO COMMENT'.UNAITWA NANI 'NO COMMENT',UMEFUATA NINI 'NO COMMENT' IPO KAZI CCM, BUTU NA UBUTU WAKE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad