Katika hao wapo waliokuwa wanajihusisha na kampeni zaidi mtandao, kwa maana ya live politics na wapo ambao walikuwa wanasoma alama za nyakati yaani ni kama wapo hawapo.
Katika group ambao walikuwa wanafanya kampeni kwenye mitandao kama INSTAGRAM, FB, Twitter kwa ujumla umaarufu wao umeshuka tofauti na awali. Katika kuthibitisha hili, unaweza kukuta post zao zinaweza kuwa na likes kama 500 hivi licha ya masaa mengi kupita jambo ambalo halikuwa kawaida. Mfano ni Blogger Mange Kimambi, Wema Sepetu, Diamond Platinumz na wengine wengi katika post zao kisiasa wemekuwa wakipata likes chache na maoni hasi kuwa wamepotea.
Hali ni tofauti kabisa kwa wasanii waliojitokeza UKAWA kama akina Aunt Ezekiel, Shamsa Ford na wenzake, clips na picha zao Instagram, Facebook, Whatsupp zimekuwa lulu. Watu wanaonyesha kuzipokea kwa shangwe kwa kupata malikes ya kutosha licha na comments za kuwatia moyo.
Huo ni uthibitisho tosha kwamba tusiishi kwa mazoea, wasanii wanatakiwa wasome alama za nyakati na hata ni maslahi basi usijiingize katika live politics kwa maana zinaua umaarufu na kukushusha labda kama uwe UMEAMUA SIASA KUWA KAZI YAKO.
Na mwisho hii, ni kama utabiri wa upande ambao unakubalika sana ambao unaweza kuwa mshindi.
Nawasilisha