Wafanyakazi waliofichua ukweli kuhusu kikao cha Dr. Slaa Serena Hotel wafukuzwa kazi

Kama mnavyokumbuka mwezi huu tarehe 1 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa aliitisha kikao cha waandishi wa habari pale Serena Hotel, ambapo mkutano huo ulirushwa LIVE na vituo vya televisheni vipatavyo vitano na radio kadhaa nazo zikarusha mkutano huo moja kwa moja.

Katika mkutano huo alitangaza rasmi kujivua Ukatibu Mkuu wa Chadema na uanachama pia wa Chama hicho na kueleza kuwa anastaafu kabisa shughuli za siasa na kwa hiyo akaeleza kuwa hana nia ya kujiunga na chama chochote cha siasa.

Hata hivyo katika kikao hicho ambapo alitumia zaidi ya saa 1 kuongea ambapo alikitumia kikao hicho karibu chote kuporomosha mashambulizi mfululizo kwa chama chake cha Chadema na vyama vinavyounda Ukawa na kumshambulia Edward Lowassa kwa nguvu zake zote na kumuita fisadi mkubwa na kukilaumu chama chake kwa kumpokea Lowassa na kupewa fursa ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Chadema kuwa ni sawasawa na kukihamisha choo kutoka chumbani na kukipeleka sebuleni.


Baada ya kikao hicho kwisha kesho yake ikatumbukizwa clip kwenye mitandao ya kijamii ambapo mfanyakazi mmoja wa kike wa Hoteli hiyo aliyatambulika kwa jina la Neema alisikika akielezea namna kikao hicho kilivyoandaliwa na kugharimiwa gharama zote na KITENGO na namna Dr Slaa alivyokuwa amepangiwa chumba katika Hoteli hiyo na KITENGO siku moja kabla na kuwa siku hiyo kabla ya kufanyika kikao hicho Dr Slaa alilala hotelini hapo akiwa na 'mchumba' wake Josephine Mushumbusi.

Dada huyo jasiri na shujaa aliendelea kueleza kwenye clip hiyo namna watu wa KITENGO wakishirikiana na idara ya usalama wa Hoteli hiyo ambavyo walikuwa wakimuingiza kwa kificho hotelini hapo Dr Slaa na mkewe pamoja na Dr Mwakyembe ambaye alikutana na Dr Slaa na kuongea naye kwa masaa matatu kabla ya kikao chake hicho na waandishi wa habari kwa kupitia 'mlango wa nyuma' ambao kwa kawaida hutumika tu na wafanyakazi wa Hoteli hiyo.

Taarifa ambazo zimepatikana ni kuwa Mfanyakazi huyo Neema pamoja na Afisa Mkuu wa Usalama wa Hoteli hiyo pamoja na Msaidizi wake upande wa Usalama, tayari wamashafukuzwa kazi kwa 'maagizo' toka mamlaka za juu za nchi yetu.

Inasemekana pia kuwa wafanyakazi hao hawakupewa hata fursa ya kutoa utetezi wao kwa tuhuma hizo kwenye kikao cha Nidhamu kama ilivyo utaratibu wa kawaida wa Hoteli hiyo na ambavyo pia ni kinyume kabisa cha principle kuu ya Natural Justice ya right to be heard.

Hivyo basi kutokana na taarifa hizo za kutimuliwa kwa wafanyakazi hao kujulikana hivi sasa upo umuhimu mkubwa wa wakereketwa wa haki za binadamu,viongozi wanaounda muungano wa Ukawa na wananchi wengine kwa ujumla wao kulifuatilia kwa karibu suala hilo na kuhakikisha kuwa uonevu huo uliofanywa na serikali hii ya Sisiem dhidi ya wafanyakazi hao unakomeshwa na wafanyakazi hao warejeshwe kazini.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waache wafukuze watu kazi,wawanunue wasanii,Lkn cc wengine dhamira yetu ipo palepale,yani kila wakifanya hv ndo wanazidi kupoteza mvuto

    ReplyDelete
  2. Utatoaje siri za kazi miiko yakazi hawaijui pia kila sehemu ina miiko yake well done

    ReplyDelete
  3. Haya ni maonezi makubwa yanayofanywa wazi wazi na serikali ya awamu ya nne,hawa wafanyakazi waliofukuzwa wapokelewe na UKAWA wazunguke nchi nzima kuelezea uovu huo na wanapaswa kulindwa na wawe na uhakika kwamba mwisho wa siku yaani baada ya uchaguzi mkuu wa octoba 25 Na baada ya UKAWA kuchukua dola rasmi watarejeshwa kazini kwa kufukuzwa waliowafukuza,na pili la muhimu zaidi watakuwa MASHAHIDI muhimu upande wa jamhuri dhidi ya watakaoshitakiwa kwa MATUMIZI MABAYA YA NAFASI ZAO ZA UONGOZI,MADARAKA NA OFISI.SIKU INAKUJA NA HAIKO MBALI BADO SIKU 42 TUU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. yaani hata wakifanya kosa wasiadhibiwe kisa ukawa kwenda zako huko wametoa siri za wataja na hiyo ndo aDHABU YAO

      Delete
  4. mnalo hilo mgongoni ccm mna dhambi kubwa kumpeleka mzee wa watu na mchumba wake uhamishoni kisa;usaliti kumnunua, kumfadhili;kumfundisha uovu na unajua? mwisho wa ubaya aibu kakimbia.badala ya kwenda karatu sasa yupo ugenini kama msaliti anayesubiri hukumu.pole babu kwani ulikwisha wasahau ccm? huko uliko watakulipia kodi ya miezi miwili tuu halafu watakwambia wewe na mchumba wako muoshe sahani na masufuria ya wazungu ili kujikimu poleni sana

    ReplyDelete
  5. Sheria ya ajira na mahusiano Kazini ndicho kilichowacost zitafuteni mzisome hata mkizigoogle mtazipata sio mnaongelea ushabiki wa admin. Mtaendelea kufanywa wafuata mkumbo kwa ushabiki usio na maana.

    ReplyDelete
  6. kwa kweli hili la msaliti slaa ni fundisho kubwa la maisha kuuza utu wake kwa sababu ya pesa haramu za ccm.huyu mzee huko aliko yeye na mchumba mzee mwenzie wanasali mchana kutwa,usiku kucha siyo kujutia dhambi na uhalifu wao wa aibu kubwa,bali kuiombea ccm irudi madarakani ili warudi tanzania na apewe huo uwaziri alioahidiwa na watawala wa sasa.hayo yao,ni maombi yatakayogonga mwamba kwa sababu hii leo kabla ya uchaguzi tarehe 25 octoba 2015 mheshimiwa lowassa keshapita kwa ushindi mkubwa sana,asilimia 82 anangoja kuapishwa tuu.angalieni ccm,angalieni kwa lile ambalo mwenyezi mungu keshapanga litokee kamwe wewe binadamu aliyeumbwa na yeye huwezi kuligeuza,huwezi.naandika hivi na haya maandishi yangu muyahifadhi ili yawe kielelezo kwa kizazi hiki na vizazi vinavyokuja kwaamba,kilichoandikwa na mungu kutokea[future happening] kamwe hakitopinduliwa na mwanadamu ,narudia kamwe hila za mwanadamu haziwezi kukizuia.tujifunze.hila ni mipango ya shetani na ccm kwa sasa ni shetani tena shetani mkubwa mithili ya lusifeli.

    ReplyDelete
  7. Taratibu za kazi zinasema hivyo,lakini kuna mazingira unaweza kiuka hizo taratibu.Mfano jambazi limechukua chumba na mfanyakazi akabahatika kuona limeingia na silaha za moto,Je mfanyakazi huyu atakaa kimya eti kwasababu haruhusiwi kutoa siri za wateja?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad