Watu Kelele Fisadi Fisadi Richmond Richmond. Ninajiuliza Kwani Kazi ya TAKUKURU au PCCB ni Nini? Mbona Hakamatwi

Fisadi
Watu kelele fisadi fisadi Richmond Richmond. Ninajiuliza kwani kazi ya TAKUKURU au PCCB ni nini? Nilidhani baada ya ripoti ya Mwakyembe hawa PCCB wangeifanyia kazi kuweza kufungua mashtaka. Kama chombo kama hiki akijaona umuhimu huo ufisadi ni upi? Serikali ni ile ile ya awamu ya nne na bado ina muda wa kuhakikisha wanatumia chombo chao PCCB kupata ukweli wa Richmond mbona nayo imekaa kimya? au inaamini hakukuwepo na wizi wa kodi za wananchi? Watanzania tusichanganywe na vitu visivyo na ushahidi wa kutosha au ushahidi butu. Nadhani neno ufisadi au Richmond ni lugha ya kampeni kama ilivyokuwa "Maisha bora kwa kila Mtanzania". Achana nao wanaosema ni fisadi sikiliza Sera chagua kiongozi anayekufa. ##‪#‎Kiona‬ Mbali***
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UMEMALIZIA NA NENO ZURI SANA HAPO MWISHO KWAMBA CHAGUA KIONGOZI ANAYE.....

    ReplyDelete
  2. NDIO MAANA TUNAITWA WAPUMBAVU NA HAO VIONGOZI WALIOTULETEA UMASKINI.........WANAFIKIRI TANZANIA NI MALI YAO . EBU TUJARIBU KUFIKIRIA KWA MAKINI BILA KUANGALIA VITISHO VYAO... KAMA ITATOKEA KAMA LIBYA TUKO TAYARI...... T U M E S H A C H A!!! LITAKALOKUWA NA LIWE...

    ReplyDelete
  3. Wewe mwandishi umetumwa kuutetea ufisadi kwanguvu zote hata ukimsafisha vipi huyo mlengwa hupati kitu kura mi haki ya mtu yako mpe unaye mtetea bila kupiga kelele

    ReplyDelete
  4. Walishindiwa nini Chadema na ndo wao waliokuwa na list of shame leo wewe unataka kutuambia nini hayo maswali yako Chadema ndio wahusika na kwa nini walikaa kimya

    ReplyDelete
  5. WEE CHONGA TU,25/10/2015 UTANYAMAZA MWENYEWE.

    ReplyDelete
  6. SUBIRI MAGUFULI AINGIE MADARAKANI NDO USEME HAYA, TUOMBE MUNGU AENDELEE KUTUPA UHAI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad