ACT-Wazalendo Yafuta Mikutano Yote ya Dr. Slaa Ikihofia Usalama Wake Awapo Kwenye Majukwaa ya Kampeni

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimekuwa na mawasiliano na Dk. Wilbrod Peter Slaa, mwanasiasa nguli wa upinzani nchini, kuhusu uwezekano wa yeye kushiriki katika kampeni za Chama chetu kwa lengo la kuendeleza vita dhidi ya ufisadi nchini.

Tunamshukuru sana Dk. Slaa kwa imani aliyo nayo juu ya chama chetu na uamuzi wake wa kuikabidhi rasmi ACT-Wazalendo, mikoba yake ya vita dhidi ya ufisadi nchini.

Dk. Slaa anaamini kwamba chama chetu cha ACT-Wazalendo ndicho chama pekee chenye uhalali na uwezo wa kupambana na ufisadi baada ya chama chake cha zamani kuitelekeza vita hiyo. Dk. Slaa alikuwa ashiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi zinazoendelea kupitia jukwaa la ACT-Wazalendo.

Alikuwa aanze na Mkutano wa hadhara Mjini Iringa siku ya Jumatano tarehe 7 Oktoba 2015, na baadaye angeendelea na mikutano mingine katika majimbo mbalimbali na kuhitimisha kampeni hizo katika Viwanja vya Mwembeyanga Jijini Dar es Salaam, ambao ndio uwanja ambapo vita dhidi ya ufisadi ilitangazwa rasmi mnamo tarehe 15 Septemba 2007.

Baada ya tathmini ya kina chama cha ACT-Wazalendo kimejiridhisha kwamba hali ya usalama wa Dkt Slaa ni ndogo sana kwa sasa kutokana na vitisho mbalimbali anavyovipata.
 
Kutokana na hali hiyo ya vitisho dhidi ya usalama wake, chama chetu kimejiridhisha kuwa hakina uwezo wa kumhakikishia Dk. Slaa usalama wake atakapokuwa majukwaani.

Kwa kuzingatia maelezo ya hapo juu, chama chetu kimefuta mikutano yote ambayo Dk. Slaa alikuwa aifanye kupitia jukwaa la ACT-Wazalendo.
 
Chama kitaendelea kutambua mchango wake katika harakati za kukuza demokrasia na hasa bidii yake ya kujitoa katika kupambana na ufisadi nchini.
 
Tunamuahidi kwamba chama chetu kitaendeleza vita hii kwa bidii kubwa na juhudi zake kamwe hazitapotea.

Tunamtakia Dk. Slaa na familia yake maisha mema.
Samson Mwigamba
KATIBU MKUU
Jumatatu Oktoba 5, 2015.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MMEZIDIANA DAU MWENYE KISU KIKALI NDIO MLA NYAMA

    ReplyDelete
  2. ACT ndio chama kinachofuata katiba yao vizuri,hawapindi katiba,hawanunuliwi ovyoovyo.
    naamini hiki chama kama hawatakuwa na migongano wenyewe kwa wenyewe watashika nchi

    ReplyDelete
  3. act-wazalendo ya zitto kabwe imesimamisha wagombea ubunge 219 na zipo dalili dhahiri na za wazi angalau watapata wabunge mia moja na nane [108 ] katika bunge la tanzania lenye jumla ya wabunge 357.hii ina maana kwamba act-wazalendo kitakua ndicho chama kikuu cha upinzani bungeni na kiongozi wake mkuu zitto kabwe ndiye atakua kinara wa serikali kivuli.maono-maono-maono,zidumu fikra za kiongozi mkuu kabwe.msicheke,niko serious.

    ReplyDelete
    Replies
    1. unaota wewe!! tena mchana kweeeupeeeeeee!!!

      Delete
  4. NA KULE KIGOMA ANAKOGOMBEA UBUNGE KIONGOZI MKUU WA ACT-WAZALENDO ZITTO KABWE INAELEKEA ANAPATA UPINZANI MKALI,MKUBWA TOKA CCM NA UKAWA NA NDIYO MAANA HAONEKANI KWENYE MAJUKWAA KUWAPIGA TOUGH WAGOMBEA WENGINE WA ACT.NGUVU YA ZITTO KISIASA INA KASORO KUBWA SANA.NI ZITTO KUDAKIA NA KUYASHUPALIA MASUALA YASIYOMHUSU.HILI LIMEMGHARIMU NA LITAMGHARIMU SANA.MFANO KUMUUNGA MKONO KWA HALI NA MALI MSALITI MKUU WA MABADIRIKO NCHINI TANZANIA KWA SASA DR. SLAA.HILI PEKE YAKE MSISHANGAE LINAWEZA LIKAMKOSESHA UBUNGE KIGOMA,NAWAAMBIENI.PILI KUMCHIMBA DAVID KAFULILA [ESCROW SCANDAL HERO].ZITTO ANAPOMCHUKIA NA KUMCHIMBA KAFULILA KIPENZI CHA WATANZANIA WALIO WENGI,SHUJAA WA KUIIBUA ESCROW BUNGENI,BASI ANAJIWEKA PABAYA MNO KIGOMA. TATU KUWA KARIBU SANA NA VIONGOZI WA CCM HASA KIKWETE KWA KUUNGA MKONO SERA MUFILISI ZA CCM TATIZO LA ZITTO NI HILI:KWAMBA ANAJIONA SIKU ZOTE YUPO SAHIHI KWA KILE ALICHOKIOTA.SIASA HAZIENDI HIVYO,SIKILIZA WASHAURI NA JIPIME.MOTO WA UKAWA,NI MOTO WETU WATANZANIA WENGI, ZITTO KABWE HAJALIMAIZI HILO,KAMA SI WEHU NI NINI. HEBU TUPISHE.LOWASSA NI WA WATANZANIA NA TANZANIA NI YA LOWASSA,FULL STOP.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad