Batuli, Wema Hawaivi Tena!

Mwisho wa reli? Urafiki wa mastaa wawili wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ unadaiwa kupoteza mwelekeo baada ya wawili hao kusemekana hawaivi tena kama ilkivyokuwa huko nyuma walipoanza Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Habari kutokwa kwa mnyetishaji wetu wa kuaminika zilieleza kuwa, hali imekuwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo kwani kila wakati walikuwa pamoja huku wakivaa sare lakini sasa hakuna tena kitu kama hicho.

Baada ya kutonywa ubuyu huo, gazeti hili lilimtafuta Wema ambapo alifunguka: “Watu wanapenda kuniona nikiongozana na mtu wakati wote, jambo ambalo si rahisi. Mimi naona tupo sawa na hakuna kitu chochote kati yetu,” alisema Wema.

Chanzo:GPL

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na hawa nao hawana vioo majumbani kwao sura zimeumuka na kufubaa kama mkate au andazi lolikwandwa kwa hamira iliyo expire

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad