Breaking News: Balozi Juma Mwapachu Leo Ametangaza Kujivua Uanachama wa CCM. Amedai Chama Kimepoteza Dira

Treni ya mabadiliko inazidi kuongeza speed katika hizi dakika za lala salama. Kesho Balozi mwenye heshima tele ndani na nje ya Tanzania, Juma Mwapachu anaachana na Chama Cha Mapinduzi.

Hii ni siku kadhaa baada ya Mkongwe wa TANU/CCM Kingunge Ngombale Mwiru kukimbia ndani ya chama hicho kwa kile alichokisema CCM imechoka, hakiwezi kuleta mabadiliko hivyo ni lazima ipumnzishwe kwanza ili ipate pumzi upya.

Mwapachu ni moja wa wasomi, na balozi mwenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi. Na kwa kweli kuondoka kwake ni pigo kubwa sana kwa CCM, hasa linapokuja suala la kumanage mabalozi wa nje. Mwapachu anaheshimika sana na mabalozi wa nje hasa Marekani na nchi za Ulaya.

Treni la mabadiliko linazidi kuongeza kasi zaidi. Huku CCM hali ikizidi kuwa tete.


TAMKO RASMI LA BALOZI JUMA V. MWAPACHU.

NAJIVUA UANACHAMA WA CCM

Ndugu zangu,

Kesho ni siku muhimu katika kalenda ya Taifa letu. Tunamkumbuka marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyetutoka miaka 16 iliyopita. Nadhani ni siku mwafaka kwangu kufanya maamuzi magumu katika maisha yangu ambayo yanahusu uanasiasa wangu. Mimi ni mwanachama wa CCM tangu mwaka 1967 wakati nilipojiunga na TANU Youth League. Nimepata fursa ya kuwa kiongozi ndani ya Chama hiki. Lakini kuanzia kesho mimi si mwanachama wa CCM tena. Natoa maelezo yafuatayo:

Kwa kipindi chapata mwezi na nusu hivi sasa mmekuwa mkisoma makala zangu kuhusu msimamo na mwelekeo wangu katika masuala ya siasa za hapa nchini hususan kuhusu uchaguzi mkuu na mstakabali wa demokrasia nchini mwetu. Nyote mnatambua kwamba kuanzia mchakato wa kumpata mgombe wa Urais ndani ya CCM kule Dodoma, ambako nilipiga kambi, sijayumba katika msimamo wangu kwamba Edward Ngoyai Lowassa ndiye chaguo langu katika kampeni za kumpata Rais mpya wa Taifa letu.

Chaguo langu si ndoto wala mlipuko wa mapenzi juu ya Lowassa. Nimemfahamu Lowassa tangu miaka ya 90 nikiwa cadre wa Chama cha Mapinduzi kwa mahusisho katika majukumu ya Kichama. Lowassa amejaaliwa nuru na uwezo wa kuongoza na wa kupendwa na watu. Ni msikivu pamoja na kwamba ni kiongozi asiyependa ukiritimba na utovu wa nidhamu, iwe kwa upande wa watumishi au wananchi wenyewe. Kubwa kwake ni ucha Mungu wake ambao unamsaidia sana katika uongozi unaojali na kuheshimu utu, ukweli na uwazi. Wanaodhani au kutaharuki kwamba eti anaweza au ana hulka ya kulipiza kisasi kwa jambo lolote lile ni waongo; wanajilinda.

Lowassa ni chaguo la wengi na CCM, katika busara yake ya kumuengua katika mchakato wa kumpata mgombea wa Urais, kimedhihirisha kutokuwa Chama kinachoendeshwa kwa misingi ya demokrasia. Dalili za Chama hiki kupoteza lengo la kuwa Chama cha watu, na kuwa cha viongozi wachache zilianza siku nyingi na hasa katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. CCM kimebadilika na kuwa Chama cha makundi na migawanyiko yakupambana, si kwa malengo ya itikadi na ujenzi wa Chama, bali ya kumalizana na kutaka kufukuzana.

Lowassa angeweza kufukuzwa miaka mingi tu iliyopita! Aliweza kushinda vita hivyo kutokana na kupendwa na wengi ndani ya CCM. Hivyo, kujitoa kwake uanachama wa CCM hivi karibuni ni sahihi kabisa kwasababu CCM si Chama tena cha watu. Kimetekwa. Na mimi nakubaliana na msimamo wa Lowassa na hao waliyofuata kutoka nadani ya CCM.

Niliwahi kuandika makala katika ukurasa huu nikimnukuu mshairi mmoja wa Uingereza aliyeandika kwamba, ‘there comes a time when the door opens and allows the future in’. Mlango huo sasa umefunguka usoni mwangu na huu uamuzi wangu maana yake ni kukubali kwamba wakati mpya umewadia; ni wakati wa mabadiliko. Kuendelea kujihisi kwamba ningali mwana CCM wa kadi ni kukubali kujidanganya mwenyewe. Si sawa. Kama marehemu Baba wa Taifa alivyowahi kusema, ‘CCM si mama yangu’.

Hivyo ndugu zangu, kuanzia kesho mimi si mwana CCM tena. Nitarejesha rasmi kadi yangu kupitia ofisi ya CCM ya kata yangu Mikocheni, Dar-es-Salaam. Kwa sasa sijaamua kujiunga na Chama kingine. 

Mwenyezi Mungu anilinde.

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Karibu ukawa
    Karibuni nyote

    ReplyDelete
  2. Aamiin,M,Mungu atakulinda,Ishaallah

    ReplyDelete
  3. KWELI HIZI NI BREAKING NEWS KA BAMBE.MHESHIMIWA JUMA MWAPACHU,SALAAM.MIMI NINAYEANDIKA WARAKA HUU NILIKUA PIA MWANACHAMA WA CCM MWANZILISHI FEBRUARI 26,1977 NIKIWA MTUMISHI WA SHIRIKA LA SERIKALI KADI YANGU NIMEILIPIA HADI DECEMBER 2016,KWAHIYO NIMO KWENYE LEJA YA WANACHAMA HAI[ CHEKA KWA NGUVU].NILIIHAMA CCM MNAMO JULY 22 NA NINA KADI YA CHADEMA BAADA YA MATUKIO YA UHUNI WA KIKWETE NA MKAPA WAKATI WA VIKAO VYA MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM.SASA HIVI NI MWANA MABADIRIKO LABDA KULIKO HATA WENGI NILIOWAKUTA HUMO.NINA HASIRA KWA KUPOTEZA UJANA WANGU NDANI YA CCM AFADHALI NINGEANZIA KUWA SINA CHAMA.NAJUA, TENA, KWA MAWASILIANO YA TAKWIMU NA UHALISIA WA SIASA ZA TANZANIA, LEO HII NI MAELFU KWA MAELFU KWA MAELFU TUMEHAMA CCM WIMBI KUBWA LIKIWA MWAKA HUU BAADA YA BLACK-JULY.NIMEGUSWA SANA NA SABABU ZA MZEE JUMA MWAPACHU KUJINDOA CCM,NA HIZO NDIZO SABABU ZA MSINGI ZA WENGI TUNAOIHAMA CCM KWA SASA.JAKAYA KIKWETE NA BENJAMIN MKAPA WAMEIBINAFSISHA CCM,NI MALI YAO WANAIYUMBISHA WANAVYOTAKA.NACHEKA SANA NIKISIKIA MAJIGAMBO YA MAGUFULI,KWELI HUYU BWANA SI MWANASIASA.ANASEMA ANA MTAJI WA WANA CCM MILLION 20 WAKATI KWA SASA HAWAFIKI MILLION TATU.ANASEMA WAPINZANI WAPO MILLION TANO.HAPO UKIJUMLISHA SASA NA HESABU KABAMBE YA RAIA WALIOHAMASIKA NA UJIO WA KISHINDO KIKUU CHA MHESHIMIWA LOWASSA WANAOZIDI MILLION KUMI.KUMBUKA HAWA HAWA CCM MILLION TATU NUSU WAPO KWA MHESHIMIWA LOWASSA.MWISHO WA SIKU TAREHE 25 OCTOBA 2015 KURA ZA MAGUFULI MILLION MOJA NA NUSU[1.5 MILLION] NA KURA ZA LOWASSA JUMLISHA =1.5+5+10=16.5 YAANI LOWASA KURA MILLION KUMI NA SITA NA LAKI TANO MAGUFULI KURA MILLION MOJA NA LAKI TANO.HIFADHI HESABU HII UJE UNIAMBIE BAADA YA UCHAGUZI.KARIBU ARENA YA MABADIRIKO MZEE MWAPACHU.WEWE NI RAIA USIE WA KAWAIDA KAMA VILE MIMI, NI KIONGOZI MWANDAMIZI MWENYE HESHMA MILANGO YA KIMATAIFA,UTAKUA WA MSAADA SANA KWA MHESHIMIWA LOWASSA HUSUSANI KUHUSU UFUFUAJI WA UCHUMI NA MISAADA YA MARAFIKI WA NDANI NA WA NJE.

    ReplyDelete
  4. Iko siku watajuta kama wanatega vinafasi huko wakivikosa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kachelewa sana mbona,maana ni siku nyingi Wameomba ukweli na kuambiwa
      wao ni wanafiki wajiondoe ccm,bado kama 3 hivi,mtawasikia tu.Ccm mpya hatuna longolongo

      Delete
    2. Mmechelewa nyinyi mnaoitisha vikao vya darura kamati kuu Kila leo

      Delete
  5. Karibu sana baba...pipoooooozzzzzzzzzzz powerrrr

    ReplyDelete
  6. Ningependa Kumsikia Kikwete azungumze kuhusu hili. Kijibinafsisha mali za umma, Kutoa mali za umma kwa watu wa nje ingawa kisheria ni mali Za Watanzania. Kuwadharau, kutowaheshimu, kuwatumia na kuleta propaganda nchini ambazo zinaleta mtengamano, umaskini, chuki, inazorotesha Taifa. Badala yake kuelekea na kutumikia mataifa ya nje na kujipatia sifa nje na kuwasaliti Watanzania. Watanzania Wanalia na Rushwa, unyanyasaji, Uporaji na kuwatunukisha mataifa ya nje. Wakati Watanzania Wakihangaika kuleta demokrasia, Raisi wetu anatunukiwa sifa moja baada ya nyingine, Anapewa zawadi, anasifiwa kwa demokrasia ambayo Watanzania alioowaongoza hawaioni na hawaionji. Un inatoa Masifa tu, Sijui wanania gani.
    Tatizo kiongozi wetu ambaye ametumika kwa miaka kumi, analindwa na kujisikia hakuna Mtanzania atakayefua dafu. Hii inanishangaza tumepitaje hii miaka kumi. Uvumilivu wa Watanzania ni wa hali ya juu sana. Lakini watu wamesimama na kusema imetosha.Utu, Hekima,unadhifu, busara, na majivuno kama mwafrika mwenye utu na uhuru havipo.Ni vizuri tumefikia hapa bila vita. Lakini nawaomba wakuu na Viongozi wote kutumia busara ya hali ya juu kupita hapa bila matukio mabovu.
    Watanzania karibu wote wanajiheshimu na ni watulivu na wapenda amani. Lakini msiwasukumie mambo ambayo yataathiri utulivu huu.

    ReplyDelete
  7. 'wanatega vinafasi wakavikosa' hueleweki mpumbavu wewe boi wa mkapa au ni wewe mkapa mwenyewe?unaufahamu ukoo wa mwapachu kwa ujumla wao?kuna mwenye njaa? .hawana tamaa ya nafasi wala fedha ila kwa mfano huyu mzee balozi juma mwapachu amejitoa kuwatumikia watannzania kwa moyo wake wote.ama kweli leo hii mtu akikuita wee ccm sawa kabisa na kukuita wee chizi,geuka umwangalie vizuri,amekutukana vibaya.maana ya ccm kwa sasa ni chama cha mazuzu kikiongozwa na jopo la mazuzu mzuka fulani na fulani na matoto tundu yao fulani na fulani na hili li-fulani.

    ReplyDelete
  8. Baada ya kutoka ndio mnatoa maovu ya mtu kwanini kama ulikua na mapenzi na nchi yako usiyaropoke hayo ndani ya chamaaa watatoka wengi sanaaa mtasikia tu Tingatinga ndani ya ikulu na atawafagia wakina mr richimundi woteeee,,,,

    ReplyDelete
  9. Na bado, mafisadi wanakimbia mmoja mmoja

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad