CCM, Kuipoteza Dar es Salaam ni Kuipoteza Tanzania Nzima

Dar es Saaam ndiyo Tanzania. Dar es Salaam ndiyo kila kitu. Kioo cha Tanzania ni Dar es Salaam. Pamoja na uwepo wa majiji matano nchini: Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Tanga, lakini Dar ndiyo mwanzo na mwisho. Katika uchaguzi huu, CCM imenyanyasika vya kutosha Dar.

Kati ya majimbo kumi, saba yamenyakuliwa na wapinzani. Matatu tu ndiyo yako chini ya CCM. Kabla ya uchaguzi huu, Dar ilikuwa na majimbo saba. Wapinzani walikuwa na mawili tu. Mambo yamebadilika.

Hii inamaanisha kuwa Manispaa za Dar es Salaam zitaongozwa na wapinzani. Kwahiyo, ni kama kusema, Serikali ya Dar es Salaam itakuwa ni Serikali ya wapinzani. CCM imepokwa uongozi wake hapa Dar es Salaam. Ni jambo zito. Ni jambo la maumivu makali.

Hata vigogo wa nchi hii wanaendelea kuishi kwenye jimbo linaloongozwa na wapinzani: Kawe. Vyuo vikuu karibu vyote vya Dar es Salaam vipo Kinondoni yenye majimbo manne: Kinondoni, Kawe, Ubungo na Kibamba. Yote yamenyakuliwa na upinzani. Yaani, Dar es Salaam ipo chini ya utawala wa UKAWA.

Sauti iliyovuma kutoka Arusha hadi Mbeya; toka Mbeya hadi Mara; toka Mara sasa imetua Dar es Salaam. Yote yafanyike lakini hili la Dar linauma sana. Ndiyo maana hata mpambano wa Urais bado ni mbichi sana kwakuwa majimbo ya Dar es Salaam bado hayajatangazwa.

Kuna la kufanyika kichama mwaka 2020!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haijalishi Dar kashika nani tunataka wachapa kazi hata hao walio pigwa chini wa ccm walikuwa hawajibiki,,, hata wao wasipo wajibika wata pigwa chini vilevile tanzania sio Dar tu.

    ReplyDelete
  2. Huu ni mwanzo wa mageuzi makubwa tanzania. Kwa upinzani kuikamata miji ya dsm, arusha, mbeya, moshi na bukoba n.k. kwa katiba iliyopo ni muujiza wa kihistoria. Kwa bahati mbaya katiba iliyopo haitoi madaraka muafaka kuziwezesha serikali za mitaa kuleta maendeleo chanya. Bado yamehodhiwa na serikali kuu na wateule wa Rais k.m. wakuu wa mikoa na wilaya! Usishangae kuona kijana kama Makonda ambaye hakuchaguliwa na wakazi wa Kinondoni akiwakwaza madiwani kutokana na ukada wake wa CCM! Haya ndiyo mapambano yaliyoko mbele yetu - kuwapa wananchi nchi madaraka ya kuamua maendeleo yao kupitia viongozi waliowachagua.

    ReplyDelete
  3. Magufuli Chonde Chonde
    Ukimchaguwa Nauye kuwa waziri utapata laana ya wana ntwara

    ReplyDelete
  4. Poleni kuchagua magufuli kwa Bao kona
    Uchaguzi si halali Kwani zanzibar ushafutwa

    ReplyDelete
  5. Makonda si mkuu WA wilaya tena
    Stands kurithi cheo mropokaji mwenzie.nape huko CCM

    ReplyDelete
  6. Shehe yahaya alitabiri haya
    Mwanga mkubwa tapeli mganga WA CCM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad