Chadema Yaipa NEC siku tatu......Yawataka Watanzania Wampuuze Dr. Slaa

Naibu Katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika ametoa siku tatu kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, (NEC) kukabidhi nakala ya Daftari la Wapigakura kwa vyama vya siasa kwa ajili ya uhakiki vinginevyo watatumia nguvu ya umma kuwalazimisha kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mnyika alisema zipo mbinu chafu na njama zinazofanywa na CCM ili kukihujumu chama hicho na washirika wake na kwamba wamejipamba kukabiliana nazo.

Alidai kwamba Chadema imegundua kuwapo kwa uandikishaji wa watu kwa BVR maeneo mbalimbali nchini na kuwa njia pekee ya kudhibiti hilo ni tume kukabidhi nakala ya orodha ya daftari la wananchi waliojiandikisha kwa vyama vya siasa.

Hata hivyo, wiki iliyopita NEC ilitangaza mpango wake wa kuwaalika wataalamu wa mfumo wa Tehama wa vyama vya siasa pamoja na wale wa jumuiya za kimataifa ili kuukagua mfumo wake wa kupokea na kuhesabu kura.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Elimu ya Mpigakura wa NEC, Giveness Aswile alisema kazi hiyo itafanyika wakati wa kikao baina ya Tume na vyama vya siasa mwishoni mwa wiki hii.

Pia ilisema ipo katika hatua za mwisho kuhakiki taarifa katika daftari hilo kabla ya kulibandika vituoni na kulisambaza kwa wadau.

Licha ya kauli hiyo, Mnyika alisema: “Yanayoendelea kuhusu BVR yanadhihirisha kuwa ipo haja kwa tume kukabidhi vyama vya siasa nakala ya daftari la uandikishaji nchi nzima. Hii itatupa fursa sisi kuoanisha idadi ya waliopo kwenye daftari. “

Ataka wasimsikilize Slaa
Katika hatua nyingine, Mnyika amewataka wafuasi na wapenzi wa chama hicho kupuuza kauli zinazotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa kwa madai kuwa kiongozi huyo hivi sasa amekuwa wakala wa chama tawala.

Aliwataka wapenzi wa Chadema wamuombee akisema amelamba matapishi yake ya kuitetea CCM chama alichotumia muda wake kukipinga na kukikosoa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad