Dada yetu anaishi na HIV Tumwambie Ukweli Mchumba Wake Anayetaka Kumuoa?

Nina mdogo wangu wa kike baba mmoja ila mama ndio tofauti, mzee alikua na wake wawili.Huyu binti alikua akifanya biashara za kusafiri kwenda Kampala na nairobi kwa miaka mingi, ni mdogo wangu wa nne kuzaliwa, tupo Tisa kwa hao mama wawili, ila mama zetu hawapo duniani, mzee ndio bado yupo katika hizi safari za kibiashara bahati mbaya akapata ugonjwa huu wa kisasa, aliugua sana hapo katikati, nadhani ilikua 2006-2009.

Baadae akapona akainuka kabisa kutoka kitandani lakini akaambiwa asiache dawa za kurefusha maisha, tukamzuia kuendelea na hizo business za kusafiri, akaokoka na bado anaabudu hadi sasa, amenona hasa, amekua kipande cha mtu.Simzungumzi vibaya Dada yangu, ila kwa kweli amekua na wowowo lenye kumvutia mwanaume yeyote yule.

Nadhani ni katika muonekano huo ndipo akajitokeza mlokole mwenzie huko kanisani kwao kutaka kumuoa, huyo jamaa kachanganyikiwa na yuko resi mno, ameshaniletea barua nami nikaipokea pamoja na wenzangu, baadae tukamtajia mshenga wake mahari nayo akalipa na tulishaila, tuligawana makaka, nae binti tukampa kidogo.

Sisi hatujaanza utaratibu wa vikao ila wao upande wa jamaa walikaa vikao viwili tayari, wakati wote huu mimi nilidhani dada alishamweleza status yake huyu mchumba, na pengine nikadhani wote wana status hiyo hiyo ya HIV positive wameamua ku team up kuunda familia, kumbe sivyo huyu jamaa hajui chochote kuhusu hali ya huyu dada yangu.

Kuna dada yetu mkubwa aliempeleka kanisani huyu binti na wanasali pamoja, juzi alimuuliza muolewaji kama amemwambia mchumba hali yake, akajibu hajamwambia, anaogopa akimwambia atakosa ndoa, na yeye anahitaji kuwa na familia yake kama mwanamke, na kwamba yeye mwenyewe haachiwe jambo hilo atalimaliza mwenyewe, na kwamba tusimwambie mchumba chochote.

Roho yangu inanisuta sana kushiriki jambo hili, hasa ukichukulia kuwa nyumba na mji wangu ndio unaochukuliwa kama nyumbani kwao na bibi harusi, na tupo karibu sana kimawasiliano na huyo jamaa.Mfano ni juzi tu kanitumia laki mbili akisema ni ya chai.

Pia ni msomi mwenye carrier yake na future inayoeleweka, hivyo nafsi inanisuta, wenzangu wanadai afya za maharusi sio kazi yetu, kwamba sie kazi yetu ni kusherekea tu, kwamba ni miaka sasa hatujawa na harusi tunachangia watu tu

Wadau, nahitaji msaada wa mawazo

Au na mimi nipotezee tu watajuana wenyewe?

By Navin-govind/JF
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Maoni yangu ninavyoona mi naona sio sawa.ni,lazma aelezwe ukweli.wewe jiweke kwenye,sehemu yake angekuja,mwanaume mwenye HIV akakuficha ingekuwaje.lazma mwanaume huyo ajue na mwenyewe aamue.na mungu ataleta wepesi.alichokiandika mungu ndo kitakachokua.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad