Edward Lowassa Awe Kielelezo cha Kuigwa Katika Kutimiza Malengo Yetu

Mara kadhaa nilikuwa na mtazamo hasi juu ya mh.Lowassa Mwaka jana mwezi wa Feb nilipata bahati ya kuwa na mazungumzo na mmoja wa washauri wa masuala ya kisiasa wa chama cha mapinduzi ambaye ni proffessor mstaafu wa chuo kikuu cha Dar es salaam ninamwamini sana na ni mkweli katika mazungumzo ya hapa na pale tuligusia swala la Richmond Maelezo yake na hitimisho lake baada ya kusoma ripoti ya mwakyembe hakuona sehemu ambayo Lowassa alihusika. Tokea siku ile nilibadili mtazamo wangu juu yake kwasababu kabla nilimuona ni fisadi na mtu asiyefaa kuwa kiongozi. Japo haindoi ukweli kuwa lowassa ana uchafu wake na yeye lakini ni nani basi msafi amponde jiwe? iwe ndani ya chadema au ccm?

Pamoja na mambo yote aliyopitia nimependa ambavyo amekuwa na msimamo katika kusimamia lengo lake na hili ni moja ya sifa ambayo kiongozi anapaswa awe nayo. kuna tofauti kati ya uchu wa madaraka na kutimiza ndoto na malengo uliyojiwekea. uchu wa madaraka ni pale ambapo mtu amepewa dhamana ya uongozi kwa muda mrefu na bado anataka kuendelea hata kama wale ambao anawaongoza hawamtaki katika nafasi ile.

Lowassa aliutamani urais toka angali kijana hii ilikuwa ni ndoto yake. aliutaka kwaajili ya haya anayotuambia au kwa maslahi yake hilo jibu analo yeye na MUNGU pekee. baada ya kushindwa 1995 walijiwekea mkakati na miaka 10 baadaye Lowassa alimuachia rafiki yake na akamsaidia mpaka akawa Rais wa nchi hii, Lowassa alizawadiwa uwaziri mkuu kama njia ya kuja kushika majukumu ya Urais 2015. hapo katikati yalitokea ya kutokea na makubaliano yao yakaingia shimoni. marafiki wakawa maadui wakubwa. huku mmoja lengo lake likiwa ni kuwa Rais wa nchii hii. Rafiki yake alifanya kila jitihada kuhakikisha lengo na adhma ya rafiki yake haitimii.

Katika hatua ambazo tunaweza kusema rafiki yake ali win mchezo ni hatua za awali ndani ya chama. pamoja na nguvu ya ushawishi na wafuasi wengi lowassa hakufua dafu. pamoja na kushindwa huko bado Lowassa hakukata tamaa sababu yeye ndoto yake ilikuwa ni kuwa Rais wa nchi hii na alijiandaa kwa kila hali ili ndoto yake itimie.Lowassa akavunja mwiko ambao haujawahi vunjwa toka CCM izaliwe tena akiwa mtu aliyewahi kushika wadhifaa wajuu kabisa. Lowassa hakuwa tayari kuona mtu mmoja anakuwa kikwazo katika kutimiza ndoto yake. aliaamua kumkwepa huyo mtu ali atimize ndoto zake kwa mrango mwingine.

Lowassa alifanikiwa na Lowassa amegombea urais. Lowassa anadai ameibiwa kura kama madai yake yana ukweli mbele za MUNGU Lowassa ni Rais wa Nchi hii hata kama ataenda monduli Kuchunga ng'ombe. na kama basi ameshindwa kihalali basi lowassa atakuwa ameshindwa kutimiza ndoto yake lakini ameshindwa dakika za mwisho katika kupigania ndoto zake. hili ni funzo kubwa kwetu weka pembeni kashfa,mienendo na tabia zake binadamu wa aina yake ni wachache haswa kwenye nchi yetu.

Jipime mwenyewe ulipokuwa mtoto mdogo ulikuwa na ndoto ya kuwa nani ukiwa mkubwa? Je leo unaiishi ndoto hiyo? kama ndio hongera kwasababu wewe ni miongoni mwa wachache waliofanikiwa kuishi ndoto zao kama hapana ni ulikabili vipi changamoto zilizokufanya usitimize?.

Kama we ni mdogo basi jifunze na uchukue hatua kabla wakati haujakuacha.

Kama watanzania tunapaswa kujiuliza je Rais mteule aliwahi kuota kuwa Rais alijiandaa na kupambana kufikia ndoto hii? Kama ni kwa bahati basi tutegemee nini? na kama kweli alijiandaa na kupigania ndoto yake basi tutegemee nini kwa hili pia

 By Major Mwendwa

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Amakweli wajinga ndio waliwao, Mr. DJ Mbowe kamlia 'chake' babu wa watu huku akjua fika hafai kuwa Rais, kwa jinsi walivyomchafua majukwaani........watanzania shikamoooni, hamsahau!!!! Piiiiipooooos PWAAAAAAA

    ReplyDelete
  2. Mmh sijui,ila mimi naona tulio wengi tulikatishwa tamaa na kuamini kama kweli alikuwa na mapenzi ya dhati na nchi kwa kujiuliza maswali haya.
    .1.akiwa waziri mkuu hatukuona hata siku 1 anapanda daladala kwenda tandale au kokote kuona nini kinaendelea kwa wananchi wake.
    2.alikuwa hana muda wa kumwaga sera kama wagombea wenzie saidi ya kusoma au kuafiki kilichosemwa na akina mbowe,sumaye na wengine.
    3.mara nyingi alikuwa anasaidiwa hata kupanda jukwaa kiasi wengi kuamini ni mgonjwa na asingeweza kutuongoza ipasavyo.Mungu ampe nguvu na uhai aone nini kinaendelea baada ya yeye kuukosa urais kwani ni kweli ameipa CCM changamoto,MUNGU IBARIKI TZ.

    ReplyDelete
  3. Yote kwa yote, Rais ametangazwa, wapo wanaofurahia na wapo wanaopinga. Ukweli halisi wanao wasimamizi wa Uchaguzi kuanzia vituoni hadi makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Ni dhahiri kuwa hawawezi kuzihadaa hata nafsi zao na Mungu kwa lo lote walilolifanya iwe ni matokeo dhahiri sawa na kazi iliyofanywa na wananchi au ni uchakachuaji kwa manufaa ya waliowatuma kufanya hivyo. Ninachopenda kuwaambia Watanzania wenzangu, tuendelee kuilinda amani ya nchi yetu, na kuitafuta haki yetu kwa hali ambayo haitasababisha vurugu na kutuletea msiba wa kitaifa.

    Mungu ibariki Tanzania,

    Fadhili Kiwera

    ReplyDelete
  4. KILICHOTOKEA NI DHURUMA NA WIZI WA KURA WA HALI YA JUU.MSHINDI HALALI WA KITI CHA URAIS NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA.YEYE NDIYE ALIYEPASWA KUWA RAIS HALALI WA TANZANIA.SISI WATANZANIA WENGI TULIOMCHAGUA TUTAENDELEA KUMTAMBUA KUWA NI RAIS WETU HALALI KWA KIPINDI 2015-2020.HATUKUWAKUBALI WALA HATUKUWAPENDA WAKOLONI WA KIINGEREZA LAKINI WALITUTAWALA.HATUMPENDI WALA HATUMKUBALI MAGUFULI LAKINI ATATUTAWALA.UNAJUA KWA NINI?UPENZI WETU WA AMANI KATIKA NCHI NA KUEPUSHA SINTOFAHAMU.ILA KWA ZANZIBAR WIZI WA CCM UMEKWAMA.WANANCHI KULE WALIWAHI KUUBAINI NA KUCHUKUA HATUA.NA, TUNASEMA KWA MIAKA HII MITANO IJAYO YA UKANDAMIZAJI WA UTAWALA BATILI NA WA KIMABAVU WA CCM WABUNGE WETU AMBAO SAFARI HII WANAVUNJA REKODI YA WINGI WAO BUNGENI TOKA 84 HADI 106 WATAWAONYESHA WEZI HAWA JINSI NGUVU YA UMMA ILIVYO.MWISHO UPENDE,USIPENDE,UCHEKE,ULIE MHE.LOWASSA ALIPATA KURA HALALI MILLION 10,268,295 AU ASILIMIA 62 YA KURA ZOTE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad