Esther BULAYA Na Wafuasi 6 wa CHADEMA Watiwa Mbaroni na Jeshi la Polisi

MGOMBEA ubunge Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Esther Bulaya, amelala mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Musoma, akidaiwa kutaka kuvamia Kituo cha Polisi Wilaya ya Bunda.
Bulaya, alikamatwa juzi jioni mjini Bunda pamoja na wafuasi sita wa chama hicho, kisha kusafirishwa usiku hadi mjini Musoma. 
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya Bulaya na wenzake kuachiliwa kwa dhamana jana, wakili wa chama hicho, Peter Makole, alisema kukamatwa kwa mwanasiasa huyo ni njama zinazoendelea kufanywa na wapinzani wao ili kumdhoofisha.
Alisema Bulaya na wenzake, wamefunguliwa kesi ya kutaka kujaribu kuvamia kituo cha polisi, jambo ambalo halina ukweli.
Makole alisema Bulaya, alifika kituo cha polisi mjini Bunda juzi saa 11 jioni kwa lengo la kumuona Kaimu Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Kaunya Yohana, aliyekuwa akishikiliwa kituoni hapo ili kujua sababu za kukamatwa wake. 
Alisema Bulaya na wenzake, wanatarajiwa kufikishwa mahakamni leo. 

Kwa upande wake, Bulaya alisema hizo ni njama za kutaka kumdhoofisha katika kampeni yake ya kuwania ubunge, ambazo haziwezi kumkatisha tamaa, na kuwaomba wapigakura wa jimbo hilo kutotishwa na matukio ya aina hiyo. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philip Kalangi, hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. BRAVO!!!! BULYA TUPO NYUMA YAKO TAREHE 25 KURA ZOTE KWAKO MUNGU NI MWEMA UTASHINDA!!!!

    ReplyDelete
  2. SISIEM MAJI YAMWESHAMWAGIKA HAYOZOLEKI

    ReplyDelete
  3. Pole dada yangu
    Mwisho wao karibuni
    Na wala Hakuna visasi nao

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad