Full Time ya Arsenal Vs FC Bayern Munich na matokeo ya mechi nyingine za UEFA October 20 (+Video)

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea leo October 20 kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya. Miongoni mwa mchezo uliyovuta hisia za mashabiki wengi wa soka ni mchezo kati ya Arsenal dhidi ya FC Bayern Munich yaUjerumani ambayo kabla ya mchezo huo kumalizika ilikuwa haijapoteza mechi hata moja.
Screen-Shot-2015-10-20-at-23.46.29
Kikubwa kilichokuwa ni kivutio cha mechi hiyo ni mashabiki wa soka walitaka kuona kamaArsenal ingevunja rekodi yake yenyewe, Arsenal ambayo ilikuwa imeshapoteza michezo miwili ya awali, ilikuwa haijawahi kupoteza mechi tatu mfululizo za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Klabu ya Arsenal ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani imeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya FC Bayern Munich.
1570
Mchezo ambao ulikuwa hukichezwa kwa tahadhari kwa timu zote hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika kulikuwa hakuna timu iliyokuwa imeona nyavu za mwenzake.Arsenal ambayo ilikuwa na wakati mgumu wa kutaka kufufua matumaini ya kutaka kufuzu hatua ya 16 ilianza kupachika goli dakika ya 77 kupitia kwa Olivier Giroud kabla ya dakika ya 90 Mesut Ozil kuhitimisha kwa kufunga goli la pili.
2111292_heroa
re
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizochezwa usiku wa October 20
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad