Mapema wiki hii, watu wasio na nia njema walitengeneza mfano wa gazeti la Mwananchi kwenye mitandao ya kijamii likionyesha habari ya kumchafua Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa umoja wa vyama vinavyounda Ukawa, James Mbatia.
Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen, imelaani vikali upotoshaji wa makusudi unaolenga kutumia jina la Mwananchi kuwachafua wanasiasa na watu wengine hasa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Mapema wiki hii, watu wasio na nia njema walitengeneza mfano wa gazeti la Mwananchi kwenye mitandao ya kijamii likionyesha habari ya kumchafua Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa umoja wa vyama vinavyounda Ukawa, James Mbatia. Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu alishauri timu za kampeni za vyama vyote, kunadi sera zao na kuonyesha jinsi watakavyozitimiza badala ya kusambaza propaganda zinazolenga kuchafua jina la kampuni ya Mwananchi. Alisema MCL inapanga kuwasilisha malalamiko rasmi kwa vyombo vya sheria ili vichukue hatua kutokana na udhalilishaji huo.
Hii si mara ya kwanza kwa watu wenye nia mbaya na magazeti ya kampuni ya Mwananchi kutengeneza mfano wa gazeti na kuandika vichwa vya habari ambavyo vina lengo la kuichafua.
Machumu alisema ingawa MCL haihusiki kwa vyovyote vile na gazeti feki hilo lililokuwa linasambaa kwenye mitandao, inamuomba radhi Mbatia na wengine wote walioumizwa na kitendo hicho
Gazeti la Mwananchi Lafunguka Vikali Kuhusu Kumchafua James Mbatia Kwa Mfano wa Gazeti la Mwananchi
2
October 03, 2015
Tags
Hivyo mwananchi ni gazeti au kijarida tuu!
ReplyDeleteIfike wakati watanzania tuwe na hofu ya Mwenyezi Mungu na kutenda haki. Kwani haki ndiyo itakayotuweka pazuri na SI KUCHAFUANA. Hiyo si maana ya siasa watu kuchafuana tena kwa kutumia vyomvo ambavyo TUNAVIAMINI. Bora Mwananchi mchukue HATUA ILI HAO WATU WAKIBAINIKA WAADHIBIWE VILIVYO.
ReplyDelete