Jana asubuhi alifika mtaalamu wa ndege kutoka Afrika Kusini na kuirusha hadi Dodoma Mjini.
“Ni kweli kuna tatizo hilo na hadi sasa (juzi) tunasubiri mafundi kutoka Dar es Salaam ili waje kuikagua na kujua tatizo lake nini,” alisema Lusinde, ikiwa ni siku moja baada ya helikopta nyingine kuanguka na kuua abiria wanne akiwamo mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe.
Kutokana na hali hiyo, Lusinde alisema, “Hata wakinipa ndege nyingine siwezi kuitumia tena, nimeamua kuwa ardhini na kama kufa bora nifie chini lakini siyo angani. Nasema katika kampeni hizi situmii anga tena na sababu kubwa ni kuwa zaidi ya wananchi wangu 500 wamepiga simu kunisihi nisitumie usafiri wa anga kipindi hiki”. Mgombea huyo ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na mmoja wa wajumbe wa timu ya kampeni za mgombea urais wa chama hicho, alisema wakati ndege hiyo ikishindwa kuruka alikuwa amefanya mikutano mitatu jimboni kwake na alitarajia kumaliza kisha kuendelea katika mikoa aliyopangiwa kumnadi Dk John Magufuli.
Aliwataja waliokuwamo kwenye helikopta hiyo kuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Chamwino, Devotha Mbogoni; Katibu Mwenezi wa CCM wilaya, Marietha Mkuya; Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Mvumi Mission, Mathias Lusano na yeye na kwamba, wote walitoka wakiwa
CHANZO MWANANCHI