Idd Azzan Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni Apigwa Chini na Wapiga Kura..Wadai Imetosha! Sasa CUF Yakabidhiwa Jimbo

Wimbi la vyama vya upinzani kushinda ubunge jijini Dar es Salaam limeendelea baada ya mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo katika jimbo la Kinondoni, akimshinda mgombea wa CCM, Idd Azzan.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo, msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo ambaye pia ni mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Mussa Natty amesema, Mtulia amepata kura 70, 337 huku Azzan aliyekuwa anatetea kiti chake akipata 65,964.

Kwa matokeo hayo, Kinondoni linakuwa jimbo la pili kunyakuliwa na chama hicho katika matokeo rasmi ambayo yamekwishatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) baada ya kulitwaa jimbo la Temeke lililokuwa linashikiliwa na mwanasiasa mkongwe, Abbas Mtemvu mapema jana.

Ushindi wa chama hicho, unafuatia ule ulioandikishwa na Chadema kwa kunyakua majimbo ya Kawe, Ubungo, Kibamba na Ukonga, hali inayoashiria kuimarika kwa nguvu za vyama vya upinzani jijini Dar es Salaam hasa vilivyo chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Kwa mujibu wa Nec, CCM imeibuka vinara katika majimbo ya Ilala, Kigamboni na Segerea huku matokeo ya jimbo jipya la Mbagala yakiwa hayajatangazwa.

Hadi jana, Nec imeshatangaza matokeo katika majimbo 194 ambapo CCM imeshinda viti vya ubunge katika majimbo 135, Chadema majimbo 34, CUF majimbo 23, NCCR-Mageuzi jimbo moja na ACT-Wazalendo jimbo moja.

Hadi Nec inaahirisha utangazaji wa matokeo jana, mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli alikuwa anaongoza kwa kura 2, 461, 771 sawa na asilimia 57.21 huku mgombea wa Chadema, Edward Lowassa akifuatia kwa kupata kura 1, 764, 785 sawa na 41.01.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bora watoto wapumzike kuwa punda wa kubeba unga

    ReplyDelete
  2. Bora na punda wapungue huko Kinondoni aisee

    ReplyDelete
  3. Safi sanaaaaaaaaaa,hayo ndio mabadiliko tunataka.
    Mnawaharibu watoto wetu kwa sembe halafu tukupe kura kisa mimi ni CCM.duh,kwa imani yangu hata Mungu atanilaani,nilisema Nooooooooooooooooo!nikakuchinja na kura yangu ikaenda upinzani.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad