January Makamba Adai Magazeti Yanampendelea LOWASSA Kwa Kumpigia Kampeni

Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba ameonesha kutokubaliana kwake na ripoti za kinachojili kwenye mikutano ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa na kueleza kuwa  Magazeti hutumiwa kupiga kampeni.

Makamba ameeleza hayo kupitia mtandao wa Twitter baada ya mtu mmoja anaetumia jina la ‘Gachanja Muigai’, kumueleza kuwa kutokana na kile wananachokisoma, inaonekana kuwa wananchi wengi wanamuunga mkono Lowassa. Na akataka kupata maoni ya Makamba kutokana na hali hiyo kama anadhani wataweza kushinda.

“@JMakamba @MagufuliJP From what we read here, it seems #Lowassa is resonating with Wananchi. Una hakika si wakati wa kuvuka sakafu?” Aliuliza.

Makamba alimjibu kuwa wapinzani wanatumia baadhi ya magazeti kama sehemu ya kampeni zao lakini tafiti na hali halisi nchini inaeleza tofauti.

“They’ve turned some newspapers into their campaign fliers. But the polls & mood across Tanzania tell another story.”

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kazi ipo Mwaka huu

    ReplyDelete
  2. Sasa jmn mbona star tv na tbc. Wanampendelea magufuli au haangaliagi au ndio mkuki kwa.

    ReplyDelete
  3. Hata Picha January
    Msidanganye watu CCM
    Watanzania wana macho Na wengi watutumia toka whatsapp
    Picha za CCM Na Ukawa
    Tu we wakwele jamani
    Mbona Ukawa hawalaamiki Picha zenu
    Mna matangazo Kila mtandao hadi vyooni

    ReplyDelete
  4. kila nikimuona januari makamba kwenye vyombo vya habari ninakua nimeiona picha ya kijana muongo,mwizi,muhuni,tapeli,aliyejawa husuda,mchimvi,bazazi,hayawani,hamnazo,kimbelembele,mponza watu,kibaka,mpiga chabo na makwapukwapu.ni mjinga sana.mfano mdogo tuu.ccm ina radio-radio uhuru-inayobebwa na serikali na kusikika nchi nzima.ccm ina gazeti lake -uhuru.niwaambieni tangu mheshimiwa lowassa anaanza kampeni tarehe 29 august 2015 hadi leo tarehe 15 octoba 2015 si uhuru radio si uhuru gazeti wamewahi kutoa habari inayohusu kampeni ya mheshimiwa lowassa,hata kwa sentesi moja,hata kwa msitari mmoja.wao lowassa ndiye jinamizi wao nambari moja.wasichokifahamu kwa ujinga na unafiki wao ni kwamba MAANA YA NENO LOWASSA NI =MUUNGANO WA WATANZANIA WALIO WENGI [MAJORITY] KATIKA KUHAKIKISHA WANAING'OA CCM MADARAKANI HAPO JUMAPILI TAREHE 25 OCTOBA 2015 KWENYE KUPIGA KURA.hii ndiyo maana halisi ya jina au neno LOWASSA.

    ReplyDelete
  5. maji yameshawafikia shingoni hawa hawana jipya, hata kuiba kura mwaka huu naona wanaiona ni ngumu!! ndiyo maana wanatapatapa!!

    ReplyDelete
  6. mimi naomba wajiaminie hivi hivi kwamba huo umati c wakweli, ili wasifanye mbinu za kuiba kura, wakione cha mtemakuni!!

    ReplyDelete
  7. Hivi haiwezekani kwao kufanya maongezi bila kumtaja Lowasa? Kweli Lowasa ni shigdi shiiiidaaaa

    ReplyDelete
  8. Mtoto mdogo para hadi mgongoni
    Kwa ajili ya uwongo na unafiki

    ReplyDelete
  9. Hv tunapojitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya siasa inamaanisha kuwa tunawakubali wagombea wa vyama hivyo au inaonesha kuwa sasa wa Tz tumeamka na tunakwenda kusikiliza sera ili tuchambue pumba n zp na mchele n up? coz kwa sasa story n uliona watu walivyoo jaa my b Mtwara? huyo ndo rais. sisi tunasikiliza kura wingi wetu kwenye mikutano siyo kwamba tunawaunga mkono noooooooooooooooooooooo tunataka tujue mtatufanyia nini? SUBIRINI 25, October.

    ReplyDelete
  10. Huyu ni mchonganishi an ambaye anatafuta sababu za kuleta vurugu hapa nchini.. tegemeo lao sana ni kuwatumia polisi kupiga raia wasiokuwa na makosa,,,, OLE WAO

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad