Jerry Silaa Aandika Haya Kuhusu Ajali ya Helkopta ya CCM..Kumbe Baba yake Naye Yumo Katika Hiyo Ajali


Jerry Silaaa Ameandika Haya Katika Ukurasa Wake wa Instagram

@jerrysilaa - Baba yangu Capt.William Silaa akiwa na Mhe.Deo Filikunjombe na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya helicopter 5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa. Taarifa za mwisho ilionekana imeanguka kwenye msitu wa Selous. Hakuna mawasiliano ya simu. Usiku kucha vyombo vyote vya serikali vimeendelea na jitihada za kufika eneo la tukio na jitihada kubwa zaidi zinaendelea asubuhi hii.
Nawaomba wote kuwa watulivu kwani jambo hili linahitaji umakini wa hali ya juu na ushirikiano wa taasisi nyingi za wizara tofauti.
Tuwaombee wote Mungu awanusuru. 

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad