JOYCE KIRIA Kashindwa Kuvumilia...Awapa Mchambo wa Nguvu Watu Wanaomponda na Elimu yake

'Matusi yenu kwangu ni Elimu yangu ndogo ya darasa la saba! 
Ivi ni watanzania wangapi wameishia la saba? Ivi ni watanzania wangapi hawajafika hata darasa la saba? Ivi ni Watanzania wangapi ni maskini walioshindwa kuwapa Elimu watoto wao?
Haya kwa nyie wasomi uchwara! Ivi wasomi wa Taifa hili wameisaidiaje nchi yetu?
Ivi ni wasomi wangapi wanadigrii na hawana kazi iwe ya kuajiriwa au kujiajiri?

Ivi kusoma ni kutukana watu na kuwadhalilisha huku unatamba wewe ni msomi!!! Nini maana ya Elimu? Ivi ukisoma na kuwa rais unakuwa na Haki kuwatukana wanyonge? Hadi Rais anatukana???? Ngachokaaaaaaaaa

Baba Lowassa anajua fika hata mnaojinadi mmesoma, lakini nyie ndo mambumbumbu! Yuko tayari kujenga upya Kizazi cha Taifa letu kwa kuwapa Elimu Bora sana!
Ndo Maana tunaotukanwa hatujasoma tumeamua kufanya Mabadiliko bila woga ili kila Mtanzania apatiwe Elimu Bora itakayoweza kuleta Maendeleo katika Taifa letu! Elimu ya Kufanya Maendeleo, tuachane na Elimu ya kutukana watu bila sababu! 

Tumebakiza siku 5 tuu tuingie Kanani kila mtu atasoma bure! Elimu Bora! Amen
Tangazo tangazo! Kwa Mimburula na misukule Hii ni page yangu, naandika nikitakacho! Makelele yako peleka kwenye acc yako, vinginevyo ntakunyoosha kama kawa! Mimi ni binadamu wa kawaida kama wengine kipaji cha uvumilivu sina unikomeeeeeee mxiuuuuuuuuuuu
Sitembelei nyota ya mtu yeyote! Ni mimi na Mungu wangu tuu!' Joyce Kiria

Top Post Ad

Below Post Ad