Mwanasiasa mkongwe na miongoni wa waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru jana alihutubia katika jukwaa la kampeni za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kusema chama tawala kimeishiwa pumzi.
Katika mkutano wa kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa katika viwanja vya Sinoni, mkoani Arusha, Kingunge alisema wale wote wanaohoji uamuzi wake wa kuihama CCM atawajibu hivi karibuni.
Huku akijinadi kuwa ni mwanabadiliko tangu kuasisiwa kwa CCM, mwanasiasa huyo mkongwe nchini alisema sababu zinazoonyesha kuwa chama tawala kimeishiwa pumzi ni kudorora kwa uchumi ambao kwa sasa unakuwa chini ya asilimia saba.
“Hivi karibuni hasa awamu hii ya sasa kuna dalili kuwa baada ya CCM kukaa madarakani kwa nusu karne sasa imeanza kuishiwa pumzi. Rais Kikwete amerithi uchumi ukiwa unakuwa kwa asilimia saba…sasa kwa mujibu wa serikali yenyewe unakuwa kwa chini ya asilimia saba. Uchumi sasa unadorora.”
Baada ya kushuka jukwaani, mgombea urais Edward Lowassa alipanda jukwaani na kuwataka wananchi wasichelewe kumpa kura ili akashughulikie matatizo yanayowakabili ikiwemo afya, elimu, kuboresha mazingira ya biashara na kukuza kipato cha wananchi.
Lowassa alisema atahakikisha Tanzania inaendesha kilimo cha umwagiliaji na kutoa uhuru kwa wakulima kuuza mazao yote kokote atapopenda tofauti na hali ilivyo sasa.
Kingunge Apanda Jukwaa la UKAWA Kumnadi Lowassa.......Asema CCM Imeishiwa Pumzi
23
October 09, 2015
HAPA KAZI TUUUUUUUUUUUU
ReplyDeleteCCM ndio no.1
ReplyDeletemwaka huu itakuwa no. 0!
DeleteKwa wizi WA kura
DeleteUfisadi
Umbea
Ana akili zake wiki mbili atawamaliza CCM Subirini
ReplyDeleteMvua ilinyesha kwa baraka zake kingunge kumpigia debe Lowassa
ReplyDeleteYalikuwa mapenzi toka baba WA taifa toka akhera
Amen mkombozi wa. Watanzania toka mfumo fisadi WA kulinda matajiri
DeleteKuuza rasilimali zetu kwa manufaa ya vigogo WA CCM na serikali yake
Viva Lowassa viva Lowassa
kazi mpe PUNDA
ReplyDeleteMmetupandisha malori kuja kwenye mkutano halafu hamkujali kuturudisha mlikotutoa nyie nanyi ovyoo na ndio walewale
ReplyDeleteFala Nani kakupandisha lori
DeleteCCM tangu wasanii hadi malimbukeni mta panda sana malori
Kwa tamaa ya 10000
Fryuuuuuuuuuuuuuuuu
TULIOJALIWA AKILI MZEEE TUNALIFAMU HILO HATA KABLA YA BVR CCM HAINA JIPYA TEEEEEEEEEEEEEEEEEEENE CHINI YA JUA
ReplyDeleteCCM NAMBA ONE KWA UFISADI ,MAJUNGU ,MATUSI NA MIPASHO UKITAKA HAYO WE NENDA HUKO.
ReplyDeleteFISADI NAMBA MOJA MMEMKUMBATIA WA UKAWA
DeleteMabadiliko ndiyo,lakini tatizo hatutaki mabadiliko kwa rais wa kuwatuma watu, wakuandikie,wakunyanyue,wakupangie nini uonge,kumbuka ni m-jeshi mkuu atatakiwa kula sahani moja na maafande,Lowasa ataweza?mmh jamani, eti kwa lengo la kuitoa CCM madarakani tu?MUNGU IBARIKI TZ
ReplyDeleteKona wewe
DeleteKwani hata jk alikuwa nguvu ya soda mbona kamaliza
Hata risala zote za jk anaandikiwa
DeleteNa safari za Kila Leo ulaya huendani kutibiwa Kwani hatujui
Tuna Watu wetu Kila balozi
Sichagui chama bali naangalia ni nani anafaa kuwa rais.
ReplyDeletemwenye uwezo wa kufiri,uwezo wa kufanya kazi,afya njema na mwenye huruma na watanzania,huku kwetu ambako ndio mgombea wa ukawa anatoka ni shida ya maji hakuna mfano.chagua magufuli.
Anakutafuna
DeleteKwa magufuli Hakuna shida ya maji
DeleteNa ziwa Victoria pua na mdomo
Acha usenge wewe
Babu kapewa pesa ili apande jukwaani. Chezea lowassa weye
ReplyDeletePanda back wewe upewe pesa
DeleteMZEEE SAFI SANA CCM ROHO ZITAWATOKA MWAKA HUU, POLENI ACHANI HASIRA MIAKA 54,MMEFILISI NA KUWAPA NCHI WAGENI,UMEUZA NYUMBA ZA SERIKALI ,MMEUZA MBUGA ZETU ZA WANYAMA ,MMEUZA VIWANDA MMEUZA ARIDHA YOTE WATU WANAUANA MTAZAMA TU,MIKATABA MIBOVU,EPA,ESCROW,GESI NAYO SIJUI KM IPO SALAM,NBC,NMB,TBL,NYOTE MMEUZA BADO TENA MNATAKA MPEWE NAFASI MKAENDE LEE KUPOLA ,VIJANA WANAOSHABIKIA HIKI CHAMA CCM NAWASHANGAA SANA SIKU MKIAMKA KUMEKUCHA POLENI VIJANA WA TANZANIA MALI ZENU ZINAPOLWA MNAKENUA MENO KM NGIRI MPOLI EBO
ReplyDeleteCCM KWISHAAAAAAAAAAAAAAAAAA.MZEE KINGUNGE ANAMALIZIA KAZI ILIYOANZA VIZURI,IKAENDELEA VIZURI NA SASA INAMALIZIWA VIZURI SANA SANA.SIKILIZENI WATANZANIA WENZANGU,HUU UPINZANI WA MWISHO MWISHO TUNAOUPATA TOKA CCM MIMI NILIUTEGEMEA NA,MHUSIKA MKUU NI WAFANYAKAZI WA CCM WA IDARA YA PROPAGANDA.RESISTANCE HIZI HAZITOKI KWA WALE MACHIZI WADOGO WADOGO WA CCM,ILA NI HAWA WANAOLIPWA NA CCM KUPOZA WIMBI NA JOTO KALI LA CCM KUANGUKA VIBAYA SANA SANA MWAKA HUU 2015.BYE-BYE CCM.
ReplyDelete