Kingunge Apanda Jukwaa la UKAWA Kumnadi Lowassa.......Asema CCM Imeishiwa Pumzi

Mwanasiasa mkongwe na miongoni wa waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru jana alihutubia katika jukwaa la kampeni za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kusema chama tawala kimeishiwa pumzi.

Katika mkutano wa kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa katika viwanja vya Sinoni, mkoani Arusha, Kingunge alisema wale wote wanaohoji uamuzi wake wa kuihama CCM atawajibu hivi karibuni.

Huku akijinadi kuwa ni mwanabadiliko tangu kuasisiwa kwa CCM, mwanasiasa huyo mkongwe nchini alisema sababu zinazoonyesha kuwa chama tawala kimeishiwa pumzi ni kudorora kwa uchumi ambao kwa sasa unakuwa chini ya asilimia saba.

“Hivi karibuni hasa awamu hii ya sasa kuna dalili kuwa baada ya CCM kukaa madarakani kwa nusu karne sasa imeanza kuishiwa pumzi. Rais Kikwete amerithi uchumi ukiwa unakuwa kwa asilimia saba…sasa kwa mujibu wa serikali yenyewe unakuwa kwa chini ya asilimia saba. Uchumi sasa unadorora.”

Baada ya kushuka jukwaani, mgombea urais Edward Lowassa alipanda jukwaani na kuwataka wananchi wasichelewe kumpa kura ili akashughulikie matatizo yanayowakabili ikiwemo afya, elimu, kuboresha mazingira ya biashara na kukuza kipato cha wananchi.

Lowassa alisema atahakikisha Tanzania inaendesha kilimo cha umwagiliaji na kutoa uhuru kwa wakulima kuuza mazao yote kokote atapopenda tofauti na hali ilivyo sasa.

Post a Comment

23 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAPA KAZI TUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  2. Replies
    1. mwaka huu itakuwa no. 0!

      Delete
    2. Kwa wizi WA kura
      Ufisadi
      Umbea

      Delete
  3. Ana akili zake wiki mbili atawamaliza CCM Subirini

    ReplyDelete
  4. Mvua ilinyesha kwa baraka zake kingunge kumpigia debe Lowassa
    Yalikuwa mapenzi toka baba WA taifa toka akhera

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen mkombozi wa. Watanzania toka mfumo fisadi WA kulinda matajiri
      Kuuza rasilimali zetu kwa manufaa ya vigogo WA CCM na serikali yake
      Viva Lowassa viva Lowassa

      Delete
  5. kazi mpe PUNDA

    ReplyDelete
  6. Mmetupandisha malori kuja kwenye mkutano halafu hamkujali kuturudisha mlikotutoa nyie nanyi ovyoo na ndio walewale

    ReplyDelete
    Replies
    1. Fala Nani kakupandisha lori
      CCM tangu wasanii hadi malimbukeni mta panda sana malori
      Kwa tamaa ya 10000
      Fryuuuuuuuuuuuuuuuu

      Delete
  7. TULIOJALIWA AKILI MZEEE TUNALIFAMU HILO HATA KABLA YA BVR CCM HAINA JIPYA TEEEEEEEEEEEEEEEEEEENE CHINI YA JUA

    ReplyDelete
  8. CCM NAMBA ONE KWA UFISADI ,MAJUNGU ,MATUSI NA MIPASHO UKITAKA HAYO WE NENDA HUKO.

    ReplyDelete
    Replies
    1. FISADI NAMBA MOJA MMEMKUMBATIA WA UKAWA

      Delete
  9. Mabadiliko ndiyo,lakini tatizo hatutaki mabadiliko kwa rais wa kuwatuma watu, wakuandikie,wakunyanyue,wakupangie nini uonge,kumbuka ni m-jeshi mkuu atatakiwa kula sahani moja na maafande,Lowasa ataweza?mmh jamani, eti kwa lengo la kuitoa CCM madarakani tu?MUNGU IBARIKI TZ

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kona wewe
      Kwani hata jk alikuwa nguvu ya soda mbona kamaliza

      Delete
    2. Hata risala zote za jk anaandikiwa
      Na safari za Kila Leo ulaya huendani kutibiwa Kwani hatujui
      Tuna Watu wetu Kila balozi

      Delete
  10. Sichagui chama bali naangalia ni nani anafaa kuwa rais.
    mwenye uwezo wa kufiri,uwezo wa kufanya kazi,afya njema na mwenye huruma na watanzania,huku kwetu ambako ndio mgombea wa ukawa anatoka ni shida ya maji hakuna mfano.chagua magufuli.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anakutafuna

      Delete
    2. Kwa magufuli Hakuna shida ya maji
      Na ziwa Victoria pua na mdomo
      Acha usenge wewe

      Delete
  11. Babu kapewa pesa ili apande jukwaani. Chezea lowassa weye

    ReplyDelete
    Replies
    1. Panda back wewe upewe pesa

      Delete
  12. MZEEE SAFI SANA CCM ROHO ZITAWATOKA MWAKA HUU, POLENI ACHANI HASIRA MIAKA 54,MMEFILISI NA KUWAPA NCHI WAGENI,UMEUZA NYUMBA ZA SERIKALI ,MMEUZA MBUGA ZETU ZA WANYAMA ,MMEUZA VIWANDA MMEUZA ARIDHA YOTE WATU WANAUANA MTAZAMA TU,MIKATABA MIBOVU,EPA,ESCROW,GESI NAYO SIJUI KM IPO SALAM,NBC,NMB,TBL,NYOTE MMEUZA BADO TENA MNATAKA MPEWE NAFASI MKAENDE LEE KUPOLA ,VIJANA WANAOSHABIKIA HIKI CHAMA CCM NAWASHANGAA SANA SIKU MKIAMKA KUMEKUCHA POLENI VIJANA WA TANZANIA MALI ZENU ZINAPOLWA MNAKENUA MENO KM NGIRI MPOLI EBO

    ReplyDelete
  13. CCM KWISHAAAAAAAAAAAAAAAAAA.MZEE KINGUNGE ANAMALIZIA KAZI ILIYOANZA VIZURI,IKAENDELEA VIZURI NA SASA INAMALIZIWA VIZURI SANA SANA.SIKILIZENI WATANZANIA WENZANGU,HUU UPINZANI WA MWISHO MWISHO TUNAOUPATA TOKA CCM MIMI NILIUTEGEMEA NA,MHUSIKA MKUU NI WAFANYAKAZI WA CCM WA IDARA YA PROPAGANDA.RESISTANCE HIZI HAZITOKI KWA WALE MACHIZI WADOGO WADOGO WA CCM,ILA NI HAWA WANAOLIPWA NA CCM KUPOZA WIMBI NA JOTO KALI LA CCM KUANGUKA VIBAYA SANA SANA MWAKA HUU 2015.BYE-BYE CCM.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad