Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama, James Lembeli ameelezea kinachoendelea katika maisha yake ya kisiasa hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu akiwa ndani ya chama chake kipya cha Chadema.
Akiongea katika taarifa rasmi kwa wananchi wa jimbo hilo, Lembeli amesema kuwa hivi sasa atajikita zaidi katika shughuli za chama chake pamoja na shughuli alizokuwa akizifanya kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Alisema kuwa ataendelea kufanya kazi zake na mashirika ya kimataifa kama mjumbe wa Bodi mbalimbali. Pia, ataendelea kufanya kazi ya kusimamia radio yake (Kahama FM) ambayo amedai kuwa taarifa zilizosambazwa kuwa ameiuza kulipa deni la mkopo aliopewa kuendesha kampeni sio za kweli.
Pia, Lembeli amewashukuru wananchi waliojitokeza kumuunga mkono na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya maendeleo na ataendeelea kushirikiana nao kukamilisha miradi mbalimbali aliyokuwa ameanza kuitekeleza kwa juhudi zake binafsi.
Kadhalika, Lembeli amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kuwa alikamatwa na jeshi la polisi mara tu baada ya Jumanne Kishimba wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.
Kuhusu afya yake, alisema kuwa yeye ni mzima tofauti na habari zinazoendelea kuenea kuwa ni mgonjwa hasa baada ya kupata ajali ya gari na matokeo kutangazwa
Lembeli Aeleza Hatma Yake Baada Ya Kushindwa, Ajibu Tetesi Juu Yake
2
October 30, 2015
Tags
PIPOOOOOOOOOOOSSSSS PWAAAAAAAAAAAAA!!!!!!
ReplyDeleteKwisha kabisa ukawa
ReplyDelete