Lowassa Asababisha Timua Timua ITV, Baada ya Video Akiwa Dhaifu Wakati wa Kufanya Tangazo Kuvuja

Hali ni tete ndani ya kituo cha ITV kufuatia kuvuja kwa video zinazomuonyesha mgombea wa Chadema Edward Lowassa akiwa kwenye hali ya udhoofu.

Mtoa taarifa ambaye ni mtangazaji wa ITV anasema, mmiliki wa kituo hicho Reginald Mengi baada ya kulalamikiwa na Lowassa juu ya video hizo ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii, alitaka wote waliohusika kwenye utayarishaji wake wawajibike.

Anasema uandaaji wa matangazo hayo ya Lowassa ambayo yameanza kurushwa na ITV, yalichukua muda mrefu kuyaandaa ambapo Lowassa kutokana na hali yake ilimlazimu kurudia kila mara na wakati mwingine alionekana kushindwa kuongea na kukohoa sana.

Video hizo ambazo alishindwa kuongea ndo zimesambazwa na kumkera Lowassa na kukosa imani na ITV kituo ambacho inaelezwa alianza kukilalamikia kwa kupunguza habari za mikutano yake.

Mtoa taarifa anasema tayari baadhi ya watendaji wamesimamishwa kazi kwa kitendo cha kusambaza video zinazomdhalilisha Lowassa na kuonyesha udhaifu wake ambao Chadema wanajitahidi kuuficha.

Chanzo: By Naface Kutoka : Jamii Forums

Top Post Ad

Below Post Ad