LOWASSA Atoa Kauli Nzito Jinsi Atakavyoshughulikia Matatizo Mbali Mbali ya Wananchi ili Wanufaike na Uchumi Katika Muda Mfupi


Lowassa Ameandika Haya Hapa Chini Kwenye Ukurasa wake wa Facebook:

Tutarekebisha kodi ya Misitu ili iweze kuchangia zaidi kwenye pato la Serikali.
Tutaimarisha sekta ya utalii kwa kuhakikisha kwamba nchi inavuna maradufu ya viwango vya sasa. Mkakati mkuu ni kuitangaza zaidi Tanzania nje, hususan kwenye nchi za Asia na Mashariki ya Kati.
Tutadhibiti biashara nje ya nchi kimagendo maarufu kama Panya Routes (PANYA RUTI).


Tutajenga mazingira rafiki ya kodi kwa makampuni ya nyumbani ili kuwapa motisha kulipa kodi na kuchangia taifa lao. Kwa mfano, hivi sasa idadi ya watu walioandikishwa na TRA kulipa VAT ni karibu laki 5, ingawa wanaolipa ni asilimia ndogo sana.
Tutaongeza ufanisi wa Bandari ya Da-es-salaam ili iweze kushughulikia mizigo mingi zaidi na hatimaye kupata wateja wengi zaidi, hususan kutoka nchi zilizotuzunguka. Bandari zetu ni chanzo kikubwa cha mapato ya serikali.
Tutahakikisha kwamba Halmashauri zetu zinajitegemea badala ya kutegemea ruzuku kutoka serikali kuu. Lazima Halmashauri zibuni njia madhubuti za kukusanya mapato yao badala ya kutegemea serikali kuu.


Tutahakikisha kwamba mikoa mingine ya nchi yetu inachangia zaidi kwenye makusanyo ya kodi. Kwa sasa asilimia 70 ya mapato yanayokusanywa na TRA yanatoka Dar es Salaam.
Tutaongeza idadi ya walipa kodi kwa kuja na sheria mpya ambayo itahakikisha kwamba kila Mtanzania anayefikisha umri wa miaka kumi na nane anasajiliwa kama mlipa kodi na kama ana shughuli ya kumuingizia kipato, analipa kodi inayostahili bila kuonewa.
Tutaboresha mfumo wa kodi kwa lengo la kuwawezesha wananchi waone faida ya kulipa kodi kwa kuwapatia huduma za kijamii zinazoendana na kodi wanazotozwa.


Tutaongeza makusanyo ya mapato ya ndani kutoka Asilimia Kumi Na Tano (15%) ya pato la taifa na kufikia Asilimia Ishirini kama wenzetu Kenya n.k.
Tutadhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu wanaotumia vibaya mfumo wa kodi kutoa mizigo yao bandarini.
Tutahakikisha kwamba Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) inakagua gharama za uwekezaji zinazofanywa na makampuni ya nje ili kutoza kodi sahihi. Udanganyifu wa baadhi ya makampuni husababisha upotevu wa mapato ya serikali"  LOWASSA

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Viva Lowassa
    Love you
    Sio bla bla sera Na ilani
    Tumechoka nazo
    We need action
    Thanks Lowassa

    ReplyDelete
  2. Kwa hiyo kama huna uwezo wa kufungua facebook ndo basi tena. Si aseme kwenye mikutano ya hadhara? Kulikoni kwani mpaka tusome kwenye facebook. Ama kweli rais mtarajiwa ni kiboko.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unapakuliwa wewe nini
      Magufuli hapendi mgongo
      Msukuma Yule
      Kazoewa chagulaga
      Ya wanawake Na si wanaume
      Nenda Msoga

      Delete
  3. Samahani Ngoyani kwa kweli mpigania urais wote huwa na fikra nzuri ila anapo kua kitini basi, ulikua waziri sasa ulifanya nini wakati huo? nasikia eti uko tajiri sasa ulifanya nini na huo utajiri wako ili usaidie wasio jiweza? kuna mfano mmoja usemao ngombe mzima huanza kula majani anapo tolewa ndani ya upango, na yule ambae sio mzima hubaki analala tu, hata uamshe hawezi kula majani.

    ReplyDelete
  4. Push up ndio sera!!!!!

    ReplyDelete
  5. hivi kweli hii ndio mipango ya muda mfupi au......... hebu wachumi tusaidieni

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad