Mabasi Ya Zacharia Express Yapigwa Mawe kwa Ushabiki wa Kisiasa

Mabasi  mawili ya Kampuni ya Zacharia Express mali ya Pita Zacharia mkazi wa Tarime mjini yanayofanya safari zake Tarime-Mwanza  yameharibiwa kwa kupondwa na mawe kwa kile kinachoelezwa ni  ushabiki wa kisiasa.

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Lazaro Mambosasa  alisema kuwa Octoba 26, majira ya  saa tisa mchana katika kijiji cha sokoni,Kata ya Sirari,Wilayani Tarime Gari lenye namba za usajili T.562 CAP aina ya YUTONG iliyokuwa ikiendeshwa na Joseph Magazin ikitokea katika kituo cha mabasi cha Sirari kuelekea katika egesho la kituo cha  mafuta ilipigwa mawe .

Mambosasa alisema gari hilo lilishambuliwa kwa kurushiwa mawe na kuvunjwa kioo cha mbele,vioo vine vya madirisha upande wa kulia na vioo vitatu vya madirisha upande wa kushoto vyote vikiwa na thamani ya 6,500,000.

Aliongeza kuwa siku hiyohiyo majira ya saa sita mchana gari  lingine lenye namba za usajili T.925 CZM aina ya YUTONG iliyokuwa ikiendeshwa na Ezekia  Merico(32) Dereva mkazi wa Isamilo Mwanza ilishambuliwa kwa mawe na kuvunjwa kioo kimoja cha Dirisha la nyuma upande wa kulia lenye thamani ya 2,000,000.

Mambosasa alisema kuwa  Magari hayo ni mali ya Kampuni ya Zakaria Express,nakwamba watuhumiwa wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambao ni Libaya Msabi (34)mkazi wa Remagwe na Marwa Juma(17) mkazi wa Sokoni Sirari nakwamba

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad