Magufuli Kasema Chanzo cha Mgao wa Umeme Nchini ni Wagombea Urais wa Upinzani Ambao Wamepiga Dili na Kampuni za Umeme

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amesema kuwa tatizo la umeme linaloendelea nchini limesababishwa na baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani.

Mgombea huyo wa CCM aliyasema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana mkoani Lindi na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wafuasi wa chama hicho, ambapo alisema kuwa baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani ndio chanzo cha tatizo la umeme nchini kwa kuwa ‘walipiga deal’ kupitia makampuni ya ufuaji umeme.

Katika hatua nyingine, Dkt. Magufuli, alisema amepata taarifa kwamba kuna njama zinaandaliwa kwa lengo la kumuangusha mgombea ubunge Jimbo la Mtama kwa tiketi ya chama hicho, Nape Nnauye.

Dk. Magufuli aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika Jimbo la Mtama mkoani Lindi.

Alisema Nape anaandaliwa njama ili asipite katika kinyang’anyiro cha ubunge jimboni humo kwa sababu aliwataka baadhi ya wana-CCM wajivue gamba wakati chama hicho kikiwa katika mchakato wa kufanya mabadiliko.

Hata hivyo, Dk. Magufuli alisema Nape ni kiongozi mzuri ambaye endapo yeye (Dk. Magufuli), angekuwa na uwezo wa kumhamisha,  angemhamishia kwenda kugombea katika jimbo lake la Chato.

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acha uongo Dr
    Dili ni la CCM na Lubuva
    Lakini kimenuka
    Wachawi unao huko huko CCM dr

    ReplyDelete
  2. Mtama hatutaki kuteuliwa au kulithishwa mbunge
    Hilo ndo tatizo
    Hakuna mchawi Dr hapa
    Na mdomo wake huyu Nape wana Mtama tunadabu na heshima
    Chaguo letu Lowassa na ukawa

    ReplyDelete
  3. Na mchawi wako huyo aliyekuja na jina lako kwenye kiloba kwenye kamati kuu ya CCM

    ReplyDelete
  4. Nape hawi mbunge Mtama NGO

    ReplyDelete
  5. siku zote tangu kuanza kwa kampeni hizi mgombea urais magufuli amezidi kudhihirisha kwamba ana tatizo kubwa kichwani.niliwahi miaka ya nyuma kusikia kwamba huyu bwana ana matatizo ya akili,sikuamini.lakini sasa nimejionea.ni wiki iliyopita tuu magufuli aliwanyooshea kidole tanesco kutokana na tatizo hili sugu.waziri wake akampinga,ni kama mchezo wa sinema,leo hii magufuli anasema tatizo la mgao huu mkali ni wapinzani.hii inazidi kutudhihirishia watanzania zaidi zaidi wale ambao walikua bado wanamchunguza wakimpima, kwambahafai,hafai,hafai,hafai rudia hilo neno mara tano,kisha chukua hatua,mheshimiwa lowassa anakuita njo,njo,njo.ndiyo, toroka uje mwana ccm sugu ulliyekua bado masalia ya chama-mdori.

    ReplyDelete
  6. huyu anafaa kua mkandarasi tuu

    ReplyDelete
  7. Ahaaaaaaaaaaaa shidaaaa hawa mashabiki wa Ukawa bana sijui kama hospitali itapata sehemu ya kuwalaza kwani siku ya kutangaza matokeo laa wengi watazimia kama vili mashabiki wa Simba walipo zabwa 2-0 na Yanga.

    ReplyDelete
  8. Alisema mgombea john pombe magufuli mjini arusha siku 8 zilizopita kwenye hadhara ya kampeni yake kwamba Yeye Siyo Mwanasiasa na Haijui Siasa bali yeye ni Mtendaji.yaani,Mungu wangu,anasemaje? mikutano hii ya kampeni ni mikutano ya siasa,ni mikutano ya kutangaza sera za vyama,na ndiyo mikutano mikubwa ya wanasiasa kuwaomba kura wananchi.sasa bwana magufuli katutangazia watanzania kuwa yeye si mwansiasa na haijui sias,.tunangoja nini hapo? tunaye mkongwe wa siasa na sio tuu anaijua siasa bali ni mwalimu wa siasa,mheshimiwa EDWARD NGOYAI LOWASSA anaomba kura zetu.mbona magufuli katurahisishia kazi.yaani kama vile tunateremka mlima triiiiiiiiiiiiiiii.tumpe mwanasiasa wetu nguli EDWARD NGOYAI LOWASA KURA ZETU wooooooote.pale kwenye kibox angalia wapi alipo lowassa nywele nyeupe, moyo mweupe akiwa na mgombea mwenza wake Haji Juma Duni, weka tick[ V ] umemaliza,SUBIRIA NDEREMO.

    ReplyDelete
  9. yani MUNGU atusaidie watanzania, atupe Lowassa awe raisi wetu, lasivyo hali itakuwa ngumu!!

    ReplyDelete
  10. Kwa hali hii nimeamini kweli mabadiliko yanahitajika!

    ReplyDelete
  11. Wapelekee maji Chato. Acha kuchamba kutumia karatasi wakati wana Chato wanataka maji
    Kama hukuelewa njoo Msoga tutakufundisha

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad