Mgombea Urais wa CCM Dr John Magufuli Amfagilia Mwanamuziki Diamond Platnumz

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli amemmwagia sifa lukuki, mkali wao ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kutokana na ushindi wa tuzo tatu za Afrimma zilizofanyika wikiendi iliyopita nchini Marekani
Tukio hili lilitokea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mpilipili mkoani Lindi baada ya staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba kushuka jukwaani kukamua kwenye kampeni za mgombea huyo wa urais, ndipo Magufuli alishika kipaza sauti na kumsifia Diamond aliyeshinda tuzo za Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki, Msanii Bora wa Mwaka na Utumbuizaji Bora wa Video.

“Ukweli nampongeza sana msanii Diamond kwa jinsi anavyojituma na kuipeperusha vyema bendera ya taifa letu…,” alisema Magufuli huku pia akiwapongeza Ommy Dimpoz na Vanesa Mdee walioshinda tuzo tofauti katika kinyang’anyiro hicho.

Aidha, katika kampeni hizo Magufuli aliwaahidi wakazi wa mji huo kuwajengea Lindi mpya ambayo itakuwa ya neema kupitia gesi inayopatikana kwenye ukanda huo, unafuu wa vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji ‘cement’ iliyoanza kupatikana kwa bei ya shilingi 8,000 kwenye kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara, zao la korosho ambalo Magufuli alijinandi kuwa na digrii ya zao hilo.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndo sera ya CCM hiyo wanamuziki
    Watanzania mpo
    Lowassa Lowassa 25 October linda kura yako mita 200
    Kwenye nyumba tukale na kungongea matokeo
    Tu nazo kamera kuzunguka vituo vyote vya uchaguzi
    Mawala wetu Hakuna kuvuta sigara, kunywa maji, kula chakula na mawakala CCM
    Watawawekea sumuwakale ili waibe kura
    Lowassa Lowassa

    ReplyDelete
  2. Anamjuwa Nani duniani huyu
    Jidanganyeni
    Akija ulaya wanaojazana east Africa tuuuuuuuuu
    Nmewapenda ujerumani walimwingiza mjini
    250 € kisa hajapewa has kufanya onyesho
    Chezea ujerumani haji haendi tena
    Ni uk na USA ndo tunambabaikia
    Miye bure bureshi hata kwa million 2000000
    Sendi ngo. Aombe radhi kwa baba yake

    ReplyDelete
  3. Hongera tena Daimond,subiri ushindi wa CCM sasa.Mungu ibariki TZ

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad