Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli ameombwa kuwafuta kazi baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamebainika kuwa wanakihujumu kwa kumsaidia mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Katika hali inayoonesha kuwa kuna mchwa wanaokitafuna kwa kificho chama hicho, mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM mkoani Arusha, Victor Njau alimuomba Dk. John Magufuli kuwafukuza kazi mara moja watendaji ambao wanakihujumu chama hicho katika harakati hizi za kampeni.
“Kuna viongozi wanatumia magari ya CCM, wanalipwa mishahara lakini wanaendesha kampeni za kuwaangusha wagombea wa chama tawala. Tunamtaka Dk. Magufuli akishinda aanze na wasaliti hawa,” alisema.
Hii inaonesha kuwa viongozi wanaodaiwa kukisaliti chama hicho wanafahamika na tayari ‘faili’ lao limewekwa sawa wakisubiri adhabu yao mara tu baada ya Dk. Magufuli kuingia ikulu, endapo atachaguliwa na wananchi Oktoba 25, mwaka huu.
Hili sio suala geni kwa mgombea huyo wa urais kwani alishawahi kuweka wazi kuwa anawafahamu baadhi ya watu wanawasaliti kwa kumsaidia mgombea wa Chadema, Edward Lowassa. Aliwakanya watu hao na kuahidi kuwawajibisha pindi atakapoingia madarakani, la sivyo waache usaliti huo.
Mgombea Urais wa CCM John Magufuli Akabidhiwa Faili la Wasaliti Wanaojifanya Wako CCM Kumbe Wanamsaidia Lowassa
5
October 13, 2015
Tags
Hiyo imo na ni mapenzi na mtu,hata mimi ni cuf mzuri tu lakini kwa urais simkubali lowassa bora kura yangu ipotee tu,ingawa akishinda ndio atakuwa rais wangu kwa kuwa ni mtanzania.
ReplyDeleteBASI MPO HAPO HII NI KABLA CCM HAIJASHINDWA VIBAYA OCTOBA 25.HEBU FIKIRIA CCM ITAKUWAJE BAADA YA KUSHINDWA.RASHA RASHA HII INAONYESHA WAZI KUWA KILA VIONGOZI WA CCM WANAPOANGALIANA USONI WANATILIANA SHAKA.SASA HIVI HATA MWENYEKITI WAO HAWAMWAMINI NA NDIYO MAANA KILA ELEKEZO NI KWA MAGUFULI TUU.MOTO UMEANZA KUFUKUTA CCM,TUSUBIRIE NGUMI,MATEKE,KABALI,FIMBO,MISHALE,YAANI JESHI LETU LA POLISI JIPANGENI MAPEMA,CCM KUTAWAKA.MOTO,YENA SIO MBALI MAKAMANDA WENU WASIJE WAKASEMA HATUKUWAARIFU MAPEMA.HUU NU USHAHIDI TOSHA.
ReplyDeleteHehehe halo
ReplyDeleteMfa maji hutapa tapa
Kwa Lubuva mlikozoe kimenuka
Tafuteni kingine mashoga
Mwiteni. Obama, queen Elizabeth
bi Angela Na mastaa wote duniani wawepigie kampeni
Mzee ruhusa Na mkapa hawatoshi
Lakini chaguo letu ni Lowassa Lowassa na UKAWA
Bila kusahau wawekezaji Feki China, uturuki eti na Poland
ReplyDeleteHajaletewa faili la wanatukana Kila kona
ReplyDeleteWauza unga mbuge Kinondoni
Tibaijuka chenge
Utafungua mahakama ya ufisadi
Mwenyekiti WA CCM ni Nani na ameshindwa 10 years
Kinana kinara mkuu WA meno ya tembo
Wadanganye watoto mafunguo
Wewe usomi
Ushauri wa bure angalia maisha yako they only use you
WA kukaya
61 years Mtu anaacha chama kwani anashinda gani compare to wazee toka East African hawjalipwa mafao licha ya East African payed long long time ago Mkapas time
Shame you CCM
Walimu ntawashangaa wakiichagua ccm