Mgombea Urais wa CCM John Magufuli Akabidhiwa Faili la Wasaliti Wanaojifanya Wako CCM Kumbe Wanamsaidia Lowassa

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli ameombwa kuwafuta kazi baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamebainika kuwa wanakihujumu kwa kumsaidia mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Katika hali inayoonesha kuwa kuna mchwa wanaokitafuna kwa kificho chama hicho, mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM mkoani Arusha, Victor Njau alimuomba Dk. John Magufuli kuwafukuza kazi mara moja watendaji ambao wanakihujumu chama hicho katika harakati hizi za kampeni.

“Kuna viongozi wanatumia magari ya CCM, wanalipwa mishahara lakini wanaendesha kampeni za kuwaangusha wagombea wa chama tawala. Tunamtaka Dk. Magufuli akishinda aanze na wasaliti hawa,” alisema.

Hii inaonesha kuwa viongozi wanaodaiwa kukisaliti chama hicho wanafahamika na tayari ‘faili’ lao limewekwa sawa wakisubiri adhabu yao mara tu baada ya Dk. Magufuli kuingia ikulu, endapo atachaguliwa na wananchi Oktoba 25, mwaka huu.

Hili sio suala geni kwa mgombea huyo wa urais kwani alishawahi kuweka wazi kuwa anawafahamu baadhi ya watu wanawasaliti kwa kumsaidia mgombea wa Chadema, Edward Lowassa. Aliwakanya watu hao na kuahidi kuwawajibisha pindi atakapoingia madarakani, la sivyo waache usaliti huo.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hiyo imo na ni mapenzi na mtu,hata mimi ni cuf mzuri tu lakini kwa urais simkubali lowassa bora kura yangu ipotee tu,ingawa akishinda ndio atakuwa rais wangu kwa kuwa ni mtanzania.

    ReplyDelete
  2. BASI MPO HAPO HII NI KABLA CCM HAIJASHINDWA VIBAYA OCTOBA 25.HEBU FIKIRIA CCM ITAKUWAJE BAADA YA KUSHINDWA.RASHA RASHA HII INAONYESHA WAZI KUWA KILA VIONGOZI WA CCM WANAPOANGALIANA USONI WANATILIANA SHAKA.SASA HIVI HATA MWENYEKITI WAO HAWAMWAMINI NA NDIYO MAANA KILA ELEKEZO NI KWA MAGUFULI TUU.MOTO UMEANZA KUFUKUTA CCM,TUSUBIRIE NGUMI,MATEKE,KABALI,FIMBO,MISHALE,YAANI JESHI LETU LA POLISI JIPANGENI MAPEMA,CCM KUTAWAKA.MOTO,YENA SIO MBALI MAKAMANDA WENU WASIJE WAKASEMA HATUKUWAARIFU MAPEMA.HUU NU USHAHIDI TOSHA.

    ReplyDelete
  3. Hehehe halo
    Mfa maji hutapa tapa
    Kwa Lubuva mlikozoe kimenuka
    Tafuteni kingine mashoga
    Mwiteni. Obama, queen Elizabeth
    bi Angela Na mastaa wote duniani wawepigie kampeni
    Mzee ruhusa Na mkapa hawatoshi
    Lakini chaguo letu ni Lowassa Lowassa na UKAWA

    ReplyDelete
  4. Bila kusahau wawekezaji Feki China, uturuki eti na Poland

    ReplyDelete
  5. Hajaletewa faili la wanatukana Kila kona
    Wauza unga mbuge Kinondoni
    Tibaijuka chenge
    Utafungua mahakama ya ufisadi
    Mwenyekiti WA CCM ni Nani na ameshindwa 10 years
    Kinana kinara mkuu WA meno ya tembo
    Wadanganye watoto mafunguo
    Wewe usomi
    Ushauri wa bure angalia maisha yako they only use you
    WA kukaya
    61 years Mtu anaacha chama kwani anashinda gani compare to wazee toka East African hawjalipwa mafao licha ya East African payed long long time ago Mkapas time
    Shame you CCM
    Walimu ntawashangaa wakiichagua ccm

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad