Milioni Waondolewa Kwenye Daftari la Wapiga Kura Tanzania

Tume inayosimamia uchaguzi nchini Tanzania (NEC), imefuta majina ya wapiga kura zaidi ya milioni moja kutoka kwenye orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura.
Awali tume hiyo ilikuwa imetoa idadi ya wapiga kura milioni 23.7 waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu kupitia kwa mfumo wa kielektroniki (BVR).
Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema idadi hiyo imepigwa kalamu kufuatia shughuli ya kuhakiki majina ya watu wote waliojiandikisha.

Majina ya watu milioni moja, 1,031,769 waliopatikana kuwa na makosa moja au zaidi yaliondolewa.
Jaji Lubuva alisema kuwa wengine waliojiandikisha zaidi ya mara moja, wengine hawakutimiza vigezo vya kuitwa Watanzania huku waliosalia wakiwa watu waliokosa sifa nyingine muhimu.
Kufuatia shughuli hiyo , Jaji Lubuva alisema wapiga kura watakaoruhusiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao watakuwa ni watu milioni 22,251,292.

Kisiwani Zanzibar wapiga kura wapatao laki 503,193 wataruhusiwa kushiriki uchaguzi mkuu tarehe 25.
Watu 181,452 walijiandikisha zaidi ya mara moja.
Wengine 845,944 waliandikishwa na wahudumu 74,502 waliokuwa kwenye mafunzo kabla ya kuanza shughuli kuu ya uandikishaji

Aidha majina ya watu 3,870 yalibainika kuwa watu waliokosa sifa za Mtanzania.
Wakati huohuo idadi ya vituo vya kupigia kura pia vimetangazwa.
Kutakuwa na vituo 65,105 vya kupigia kura katika uchaguzi ujao.
Vituo vya kupigia kura 63,525 vitakuwa Tanzania bara huku Kisiwa cha Zanzibar kikitengewa vituo 1,580 vya kupigia kura.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mmmm hapo tayari kuna mkono wa CCM bao la mkono laanza kazi watu milioni.
    baadaye kura milioni zitakuja kusemwa zimehalibika

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad