Mke wangu Kapewa Nini na CCM? Mbona Hataki Kumsikia Lowassa na Ukawa?

Nimetumia mpaka vitisho vya talaka lakini yeye ni Magufuli na Mama Bona wa Segerea.
Nimejaribu kuchunguza lakini cha ajabu ata kwenye mikutano ya kampeni haendi, yeye ni dukani kwake asbh Mpaka jioni. Ata TV na habari hana mpango nayo.
Mbaya zaidi kawabadirisha mpaka wadogo zangu wamehamia ccm.
Kura 7za ukawa nyumbani kwangu zimepeperuka kama vumbi na ninaziona hizo zinaenda ccm.
Kikatio chake na vya wadogo zangu wamevificha ukweni.
Swali ni jee.
CCM imempa nini mke wangu jamani.

Top Post Ad

Below Post Ad