Mohammed Dewji Anataka Kuinunua Klabu ya Simba, Kuwekeza Bilioni 20

Mfanyabiashara mkubwa nchini, Mohammed Dewji ameweka wazi mpango wake wa kuinunua klabu ya Simba inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara.

Akizungumza na kipindi cha Mkasi TV kinachoruka kupitia EATV, Dewji alisema tayari wapo kwenye mazungumzo na rais wa klabu hiyo ili kukamilisha mpango huo.

Unajua kila mtu ana interest, hakuna interest ya klabu, mimi nimeona sitaki nijihusishe na klabu ambayo haitafanikiwa, ndio maana mimi nilikuwa nasema Azam itakuja kufanya vizuri zaidi kuliko Simba na Yanga na wameanza,” alisema.

Nimeongea na rais wa Simba na ameniambia nimwandikie paper. Unajua mimi nimemwambia ‘wewe unafikiria mimi nikinunua hisa 51% ya Simba, maana yake nitaipeleka wapi? Mimi ni mtu wa hapa hapa na naipenda Simba. Leo mashabiki wa Manchester United, Arsenal they don’t care klabu ya nani, wanachohitaji ni mafanikio. Mimi nimewaambia nipo tayari niwekeze bilioni 20. Leo Katumbi wa TP Mazembe ni timu yake na inafanya vizuri. Mimi nimewaambia hata nikiwekeza bilioni 20 sitaona hela, mimi na biashara mia nyingine ninapata hela.

Kwenye mpira ni mapenzi na timu basi. Tunataka kuendeleza mpira tuendeleze Simba yetu, tupate raha Simba ikishinda. Tayari nimeshamwandikia paper sasa tunakamilisha tutapeleka kama tutafanikiwa, kama ilishindika nitaanza na Mo Football Club,” aliongeza Mo.

Aliongeza, “Tuliwafunga Zamalek, watu laki mbili walikuja kutupokea na bahati mbaya watu walikufa siku hiyo, sasa baada ya kushinda mimi niliitisha mkutano, nikasema jamani tumebahatika tumeshinda lakini hebu tujilinganishe na klabu ya Zamalek. Leo bajeti yetu ni shilingi ngapi na bajeti ya Zamalek ni shilingi ngapi? Leo Simba bajeti yake ni bilioni moja kwa mwaka it’s a joke!

Mimi nimekuja na fikra nimesema kwamba jamani kwanini kuna watu wamesema wamejenga Simba? Tunawapa hisa bure za milioni 10 kila mmoja, tumefanya projection tunaweza kuraise zaidi ya bilioni 30 mpaka bilioni 40. Ukishapata bilioni 40 leo, ukienda kununua treasure bond unapata asilimia kumi tano.”

Sasa ukiwa na 40 bilioni , 10% ya 40 bilioni ni 4 na 5% ni 2 bilioni maana yake 6 bilioni. Unatoka kwenye 1 billion ya leo unaingia kwenye 6 bilioni, maana yake nini? Unaweza kumwajiri kocha mzuri, unaweza kuwa na gym pamoja na viwanja, unaweza kununua wachezaji ukashindana na Zamalek na hatimaye baada ya miaka mitano unaweza kushinda African Champions League,” alisisitiza.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad