Msimamo wa Matokeo Huu Hapa..Lowassa Achuana Vikali na Magufuli...

Wagombea wa CCM na Chadema wanaendelea kuchuana vikali kwenye mbio za urais baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza matokeo ya majimbo 113.

Hadi jana jioni kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na NEC, mgombea wa CCM, Dk John Magufuli alikuwa anaongoza kwenye majimbo mengi akifuatiwa na Edward Lowassa anayegombea kwa tiketi ya Chadema, akiungwa mkono na vyama vingine vitatu vya NLD, CUF na NCCR-Mageuzi.

Kwa mujibu wa matokeo hayo ya NEC, Dk Magufuli alikuwa amekusanya zaidi ya kura 2.4 milioni sawa na asilimia 57 katika majimbo hayo, wakati Lowassa, aliyehamia Chadema mwezi Julai, amepata kura zaidi ya 1.7 milionisawa na asilimia 41.

Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, ni NEC pekee inayoruhusiwa kutangaza matokeo ya urais.

Mgombea pekee mwanamke kwenye uchaguzi huo kati ya makada nane kutoka vyama tofauti, Anna Mghwira wa ACT-Wazalendo, anafuatia nyuma ya wagombea hao wawili, akiwa amepata zaidi ya kura27,000 ambazo ni sawa na asilimia 0.64.

Mgombea urais wa ADC, Chifu Lutasola Yemba anamfuatia kwa kuwa na asilimia 0.52 ya kura zote, chini yake akiwapo Hashim Rungwe wa Chaumma ambaye amekusanya asilimia 0.38 ya kura zote.

Janken Kasambala, anayegombea urais kwa tiketi ya NRA, amekusanya asilimia 0.09 ya kura zote, Macmillan Lyimbo, aliyesimamishwa na TLP (asilimia 0.07) na Fahmy Dovutwa wa UPDP (asilimia 0.07).

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, ambaye awali aliwahi kusema watatangaza mshindi ndani ya saa 72 baada ya kumalizika upigaji kura, jana aliwaomba wasimamizi wa uchaguzi kuongeza kasi ya kuwatumia matokeo ili wayatangaze.

Hata hivyo, vyama vinavyounda Ukawa jana vilitoa tamko la pamoja vikidai kuwa uchelewashwaji wa matokeo unatokana na uchakachuaji unaofanywa na kikundi cha chama tawala.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kura zote zinazokusanywa kutoka majimboni, hupitia hoteli moja Dar es Salaam ambako kuna kikundi hicho na vijana ambao wanachakachua matokeo kabla ya kuyatuma NEC.

Lakini Jaji Lubuva amekuwa akijitetea kuwa NEC inatangaza matokeo kadri inavyoyapokea na hawana njama zozote dhidi ya chama chochote cha siasa.

Kwa upande wa matokeo ya ubunge, CCM ilikuwa imeshinda katika majimbo 135, Chadema majimbo 34, CUF majimbo 22, NCCR-Mageuzi jimbo moja na ACT- Wazalendo jimbo moja kati ya 264.
Mpekuzi blog

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. CCM acheni ubabe. Mlikubali vyama vingi lakini bado mnaendesha nchi Kiuccm kama miungu.
    Acheni wizi na uswahili. Uswahili Wa Dar ni uswahilini. Mswahili kapewa cheo bila mafunzo ya Ustaa. Bado ni shangingi na Mswahili. Hajui tofauti ni nini. Hajalelwa na nidhamu. Kalelewa kwa bahati za mungu. Kajisikia vikubwa zidi ya tegemeo. Kalimbuka.

    ReplyDelete
  2. Replies
    1. washenzi wote hapo juu hivi hizi data nani kazisaini hiko vituoni kabla hazijafika TUME?
      hatujazoea ujinga wenu

      Delete
  3. Kwa Wazee kama nyinyi mliutundukiwa vyeo kuduguubaga, Hamjajifunza bado baba zenu walivyouzwa Uarabuni, walivyokung'utwa viboko. Mtajifunza lini Waafrika kujienzi, Kujithamini, kujitawala, Kwawaheshimu Watanzania wenzenu na kuwathamini Wato, Wanawake, Wazee wenzeu Weusi wa Taifa hili. Leo mmepewa mabawa ya kuruka juu kuwatafuta hao waliowaweka mabwana Uarabuni, Uingereza, Marekani, hamna hata Aibu nyie Wasomi kupeleka kizazi chenu tena kwa hao mahucha. Mlimwondoa Iddi Amini kumwita kibaraka na nyie ni nani. Mmepita jeshi wengine kupigania ukombozi ukombozi gani.
    Mmevaa vilemba kichwani eti kimavazi , kidini mfanane nao adabu gani za kipumbavu.Mnajiuza kama hamna thamani. Lini mtajivunia Uweusi wenu, Utawala wenu, Uhenga wenu. Kuazia Marasi, Mawaziri mnakaa majukwaani kuimba rsala ili muonekane wababe, mmejiachia mkipigwa picha na haohao mpaka machumbani mlalako hata siri za nchi hamjui kuzinadi.Ebu tengueni hayo matokeo yanayonadiwa na UN ambao wamewavisha vilemba , wanasema uchaguzi halali huku masanduku ya vema kwa kila mpigia vema wa ccm. Kuna sehemu mlijifungia chumbani Akina Makamba kuweka tiki hizo ndio maana ulianza kujinadi kabla hata ya kuanza kuhesabu. Kama nyie si mafisadi sasa nani ni fisadi.Tengueni matokeo mliojipa na kuwaheshimu Watanzania. Hii ni nchi ya Watu si mizoga yenu.
    Fanyeni uamuzi mgumu kwani Magufuli hajashinda hata. Naye yupo kimya kajificha. Toka toa cheko la kweli na si la wizi. Utakomeshaje Rushwa na uchaguzi mzima toka ulipopendelewa katika uchaguzi wa kukupata mgombea wa ccm na mambo yale yale yanaendelea kwenye uchaguzi mkuu.
    Kama ni shujaa hutakubali upandikizwe uraisi usiouweza. Ujitoe na uwaheshimu Watanzania. Utakuwa shujaa na utathaminiwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. katika watu wajinga na wapumbafu ni wewe, umeandika kitu gani hicho? hata mwanao uliyemzaa anakuzidi kufikiri na akiri jiangalie na fikiri kwanza kabla hujaandika kwa kuonekana mjinga

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad