Mzindakaya Nae Afunguka Makubwa Kuhusu CCM na Waliondoka CCM

MWANASIASA mkongwe nchini, Chrisant Mzindakaya amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wagombea wao wa nafasi mbalimbali, wasigombane na waliohama chama hicho kwa kusisitiza kwamba wakifanya hivyo, watakuwa wanakosea.

Mzindakaya alisema, CCM ni chama chenye heshima kubwa duniani na chenye Ilani ya Uchaguzi bora, yenye heshima. Alisisitiza kuwa rais bora wa awamu ya tano atatoka katika chama hicho.
Alisema hayo juzi akiwawakilisha wazee wa mkoa wa Rukwa kwenye mkutano wa kampeni ya kuwanadi wagombea urais, ubunge na udiwani kwa tiketi ya CCM uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Manispaa ya Sumbawanga.

Mkutano huo wa kampeni ulihudhuriwa na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa na Halmashauri Kuu, Mizengo Pinda ambaye pia ni Waziri Mkuu. Wengine ni pamoja na viongozi waandamizi wa CCM mkoa na wilaya.

“Sisi wazee wa mkoa huu tunasema chama cha siasa chenye heshima kubwa duniani ni CCM ambapo bila wasiwasi ndiko atakakotoka rais wa awamu ya tano ambaye ni Dk John Magufuli …
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tunajua wewe mzindakaya ni mwizi mkubwa na nikwambie umebinafsiwa rachi ya taifa ekari mia nane na benjamin mkapa.waambie watanzania uliilipa nini serikali.humo kwenye ranchi kulikuwemo na vifaa mbali mbali vikiwemo matrekta na magari.ulilipa nini mzindakaya. humo kwenye ranchi kulikuwepo na mamia ya ngombe,uliilipa nini serikali. huu ni uhujumu uchumi wa daraja la juu na shauri hili kwa kuwa ni zito zinasubiriwa mamlaka mpya tuu za dola mara baada ya uchaguzi mkuu kukamilika ambapo rais mpya wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa tanzania ,mheshimiwa edward lowassa atakapoanza majukumu rasmi kwa ile spidi 120,huponi mzindakaya. mph. kuhusu ati yeye anawawakilisha wazee wa rukwa hivi huyu mzee kwa nini anawadanganya watanzania? ni vyema akasema yeye anajiwakilisha kama yeye maana najua hata wale wafanyakazi wake kwenye ranchi hawamuungi mkono.ni mkatili sana mzee huyu copyright na mkapa. mwisho anaposema ccm inaheshimika dunia nzima mimi sielewi hilo kaliokota wapi.sasa hivi utawala wa kikwete umelitia doa taifa letu wauza unga wakubwa wanalindwa na kikwete na mtanzania yeyote anayesafiri nje atakua shahidi wangu tunasachiwa mpaka sehemu za siri,ukiwauliza wanaokusachi wanasema nchi yenu imeharibika tunawakamata wauza unga wakubwa pengine viongozi wenu wanakuja wenyewe kuwaombea msamaha kupitia ngazi za juu,wanaachiwa.hii ndiyo serikali ya ccm.wewe unasema heshima,hii ni heshima au uhalifu wa kimataifa?. k

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe anoy 3:38 umekosa kazi ya kufanya ni nani wakupoteza muda wake wakusoma stori yako ndefu kupita kiasi kama huipendi ccm hamia msumbiji

      Delete
  2. Ya CCM wana heshima ya ufisadi duniani,Hp ni kweli kbs

    ReplyDelete
  3. nihamie kwenu msumbiji nakujua wewe ni mshona wa beira msumbiji askari wa renamo muuaji uliyeyakimbia mamlaka ya dola na ni rafiki kipenzi wa mzindakaya anayefuga wahalifu,kwa sababu na yeye ni mhalifu mkubwa,hauponi mwaka huu mzindakaya .

    ReplyDelete
  4. Mapovuuuuuuuuuuuuuuuu,lakini rais wa awamu ya 5 anatoka CCM.
    UKAWA mjipange.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mjipange nyie majizi na majambazi
      Mnalazimasha magufuli ashinde grata Kama hatumtaki
      Ili alinde Mali zetu. Hatuondoki vituoni ngo kulinda kura zetu, wasimamazi wa nje wanatuunga mkono

      Delete
  5. UTABIRI :matokeo rasmi ya tume ya taifa ya uchaguzi tanzania jumatano tarehe 28 octoba 2015 ;kura za urais.idadi ya wapiga kura 12,500,000.kura zilizoharibika 75,000.matokeo ya wagombea wakuu: dr.john pombe magufuli[ ccm ] kura 1,863,400 sawa na asilimia 12, mheshimiwa edward ngoyai lowassa amepata kura 9,234,786 sawa na asilimia 84 ,asilimia 4 zimekwenda kwa wagombea wengine sita kwa mtiririko ufuatao................................................hivyo basi kwa mujibu wa sheria kifungu nambari.....tume inamtangaza mheshimiwa...............kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais 2015-2020. huu ni utabiri wangu leo hii tarehe 15 octoba zikiwa ziesalia siku tisa tuifikie jumapili ya uchaguzi mkuu tarehe 25 octoba 2015.kama kuna mwenye ubavu wa utabiri tofauti na huu,nikusome. naitwa NA-KIU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad