NEC Wasema Uchaguzi wa Tanzania Bara Hauwezi Kufutwa......UKAWA wataka NEC Nao Wafute Uchaguzi

Mwenyekiti  wa  Tume  ya  Taifa  ya  Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva  amesema  kuwa kufutwa  kwa  uchaguzi  mkuu  Zanzibar  hakutaathiri  uchaguzi  wa Rais  wa  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  kwa  sababu  NEC  na  NEC  wanaongozwa  na  katiba  mbili  tofauti.

Lubuva  ametoa  kauli  hiyo  leo  mchana  ikiwa  ni  muda mfupi  kabla  ya  kuendelea  na  utangazaji  wa  matokeo ya  Rais.

"NEC inapenda kuwatangazia wananchi kuwa kuhairishwa kwa uchaguzi Zanzibar hakutasababisha kuhairishwa kwa uchaguzi Tanzania.

"Uchaguzi wa Zanzibar unasimamiwa na ZEC na uchaguzi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani unasimamiwa na NEC, ni katiba mbili tofauti

"Uvumi unaoendelea kwamba uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umefutwa ni upotoshaji na si kweli, haujaathiriwa na lolote.
 
"Tuko hapa muda huu kuendelea na utoaji wa matokeo ya awali kama ambavyo tumekuwa tukifanya." Alisema  Lubuva  na  kuendelea  na  zoezi  la  kutangaza  matokeo  hayo.

Msikilize  Jaji Lubuva  akiongea


UKAWA  Wapigilia msumari
Akizungumzia  sakata  la  uchaguzi  mkuu  kufutwa  huko  Zanzibar,Mwenyekiti  mwenza  wa  Ukawa,James  Mbatia  amesema  kuwa  tume   ya  uchaguzi  ZEC  imeamua  kuyafuta  matokeo  hayo  baada  ya  CCM  kushindwa  vibaya.

"ZEC wameamua  kuufuta  uchaguzi  mkuu  Zanzibar  kwa  shinikizo  la  serikali  ya  Kikwete  na  CCM  yake  baada  ya  Maalim Seif  Sharif  Hamad  kuibuka  kidedea.

"Huwezi  kufuta  uchaguzi  wa  Zanzibar  ukaacha  uchaguzi  wa  Jamhuri  ya  Muungano

"Unaposema  Dola  ya  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  kwa  mujibu  wa  Katiba  ni  Tanganyika  na  Zanzibar

"Upande  mmoja  wa  Jamhuri  ya  muungano  umefuta  uchaguzi, tena  wametamka  kufuta  uchaguzi  mkuu.Sasa  kama  upande  mmoja  umeshafuta, upande  mwingine  unasubiri  nini?

"Huu  ni  mgogoro  mkubwa. Kitendo  cha Damian Lubuva  kuendelea  kutangaza  matokeo  ni  sawa  na  kiini  macho, anajifurahisha  tu  mwenyewe  na  ni  kinyume  cha  katiba." Amesema  James Mbatia
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad