Nimegundua Mzee Kingunge ni Jasiri Sana Kwa Hili Anahitaji Anahitaji Kupongezwa

Nilichojifunza katika mahojiano ya Tido na Kingunge, ni kwamba mzee huyu anaujasiri, ambao mwanzo sikuujua. Simkubali Lowassa lakini pia siwezi kukubali anyimwe fursa bila kufuta taratibu. Hata hivyo nimejifunza mambo saba ambayo ninapenda kuwashirikisha.

1. Kikwete na kundi lake walitumia hila katika kimtoa Lowassa katika kinyang'iro cha urais ndani ya CCM.

2.CCM iliwadhalilisha wagombea urais ndani ya CCM kwa kuacha kuwasikiliza na kuwahoji.

3. Kikwete na kundi lake walivunja katiba ya CCM makusudi ili kumdhibiti lowassa, na hawakutoa fursa ya kukata rufaa sababu NEC ilikuwa inamkubali Lowassa, na CC inakatiwa rufaa kwa NEC sababu ndio kikao kikubwa.

4. Maguful pamoja na uzuri wake ameingia doa baada kupata fursa hiyo kwa njia ya mizengwe badala ya utaratibu wa chama.

5.Ufisadi wa Lowassa unakosa mashiko kuzungumzwa na CCM, chama ambacho kina dola ndio chenye wajibu kukamata na kupeleka mahakamani.

Hii ina maanisha huenda Lowassa hausiki kabisa na Richmond au kufikishwa kwa lowassa mahakaman ndo mwanzo wa Kikwete kuondolewa kinga ya kutoshitakiwa.

6. Kingunge ni mtu ujasiri sana kwa kitendo chake cha kutafautiana na wenzake endapo taratibu walizojiwekea zikivunjwa. amethubutu kupingana na Nyerere, mtu ambaye ilitaka ujipange kabla ya kufikiria kumpinga.

7. Hili ni la mwisho lakini ni la kwanza katika umuhimu. Kikwete kama mwenyekiti wa CCM amevunja katiba ya CCM.

Pamoja na hayo lazima tujue akili na busara ndio zilizozaa katiba na kanuni zake za uendeshaji, ni wajibu kufuata katiba lakini ni wazimu kudhani KATIBA ni bora kuzidi BUSARA iliyitumika kutengeneza katiba.

Kama ndivyo, ni sawa kiongozi kujitia wazimu na kupindisha vifungu vya katiba, ili mradi afanye hivyo kwa maslahi ya watu wote wanaongozwa na katiba husika. Asulubiwe kwa kuvunja katiba lakini mafanikio ya uvunjaji huo kuyabeza ni ujununi.

Mwalimu Nyerere aliunganisha TANU na ASP kwa kuvunja mkataba wa muungano, lakini alifanya hivyo kwa lengo kuwa na chama cha kitaifa kitakacho tuunganisha sote bila kuzingatia utanganyika au uzanzibar, amefanikiwa katika hili na katu hatuwezi kubeza.

Je, kikwete kavunja katiba ya CCM kwa maslahi ya wanaCCM wote au kwa maslahi yake na mtandao wake? sio mwanaCCM kwa hivyo jibu sina.

Njano5
0784845394

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kikwete kavunja katiba ya CCM kwa maslahi yake na mtandao wake na sio mwanaCCM . CCM isipochaguliwa mwaka huu itabidi Kikwete na kundi lake wawajibishwe kwa kukihujumu CHAMA CHA MAPINDUZI NA SERIKALI YA TANZANIA... WAPIGWE MAWE MPAKA KUFA!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. pumbafu huna akiri, upigwe kwanza wewe ndo wafuate wengine, na bado mtanyooka mshenzi mkubwa

      Delete
    2. Mtaipata CCM

      Delete
    3. Pumbavu wewe mwenye kula mlo mmoja na kushabikia CCM , njaa tupu

      Delete
  2. ccm ni chama cha hila na fitina

    ReplyDelete
  3. Meno yameng'oka ukiwa ccm,sasa saa 12 ndio unataka kutudanganya ccm mbaya kisa swahiba wako kakatwa,mapungufu ccm hayajaanza leo kwa nini hukujitoa na kwenda vyama pinzani wakati huo?SIDANGANYIKI NG'O!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa sababu ni kazi ya majizi ya CCM

      Delete
    2. HAPA KAZI TU.

      Delete
    3. Mpe mkeo utajuwa mapengo yake

      Delete
  4. Kama kuvunja katiba ya ccm alianza nyerere mwaka 1995, na kama kuwajibishwa angeanza kuwajibishwa nyerere, Kingunge hana chochote cha kutuambia, huo ni uswahiba wake tu kwa lowasa, pumabvu sanaaaa...tupa kuleeee

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtaondoka mmoja mmoja mwaka huu laana toka kwa mungu
      Tukaneni

      Delete
  5. Daah, makapi hayaaa balaaa sijui ni nani aliyewaroga watanzania hadi wakayasadiki makapii. Nadhani wananchi wamechoka na amani na utulivu ndo wanataka kujaribu vita.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kapi wewe tena nasikitikia mama yako alokuzaaaaaaaaaz

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad