Rais Jakaya Kikwete amesema watu wanaopanga kubaki katika vituo vya kupigia kura baada ya kumaliza zoezi hilo kwa lengo la kulinda kura kunaashiria uvunjaji amani, hivyo serikali imejipanga kupambana na hali hiyo siku ya uchaguzi.
Rais amesisitiza kwamba wanaopaswa kulinda kura ni mawakala pekee na si wafuasi wa mgombea ama vyama.
Akizungumza jana katika sherehe za Kilele cha Mwenge wa Uhuru zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kiongozi huyo anayemalizia muda wake madarakani alisema viongozi wanaowaagiza wafuasi wao kulinda kura wana nia mbaya dhidi ya amani ya nchi.
“Mnatakiwa muondoke kwenye vituo baada ya kupiga kura….kura utazilindaje? Mawakala ndio pekee wanaoweza kulinda. Mkikaidi hilo, hatutawavulimia. Serikali imejipanga kupambana na wale wote watakaokaidi agizo la Tume ya Uchaguzi (NEC),” alisisitiza Rais Jakaya Kikwete.
Katika shehere hizo za mwenge zilizoendana sambamba na maadhimisho ya siku ya kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete aliwataka Watanzania kuchagua watu waadilifu ambao wana dhamira ya kupambana na rushwa kwa vitendo.
“Tumchague mtu ambaye hana ukabila, udini na ubaguzi wa rangi…tumchague kiongozi atakayetetea maslahi ya makabila yote 126,” alisema rais huku akimnukuu Mwalimu Nyerere aliyefariki miaka 16 iliyopita.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa pia na Spika wa Bunge anayemaliza muda wake, Anne Makinda, wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa ngazi tofauti serikalini na kupambwa na nyimbo za makabila na wanafunzi wa shule mbalimbali mjini Dodoma.
Rais Kikwete Awaonya Wanaopanga Kulinda Kura Vituoni
10
October 15, 2015
Tags
Hata hao wanaokupa medali ni wapumbavu
ReplyDeleteHufai hufai
Shame on you
Tatizo lipi mtu kulinda kura yake
Mitambo ya uchaguzi ni fekikikiji
Mtaiba kuraaaaaAaaaaaaaaaaaaaa
Ukikaidi utapigwa tuu
DeleteKwahiyo mkilinda ndio hamtaibiwa??!! Kura zinapigwa ndani, nyinyi kwa 'upumbavu' wenu mnalinda nje tena mita 100............are you serious?? Au mtatumia skype....lakini poa tu, hao 'wajeda' wote ni wageni, wamepewa mafunzo ambayo hawaja ya'practice' mtakuwa mmewasaidia sana kujipima kama 'wamekwiva'.......ASIYESIKIA LA MKUU, HUMPATA MAKUU
DeleteKumbe medali za JK winawauma roho...SAGA CHUPA UBWIE.
DeleteKama mnajua mitambo ni feki na mtaibiwa kura, kuna haja gani ya nyinyi malofa kufanya kampeni? Chunga mdomo wako, kwani mdomo uliponza kichwa
Wacha wavae sare Kila kukicha wanabadili sare
ReplyDeleteBora pesa mngeleka hospitalini
Shame you CCM
Tuchague CCM tunaumwa
Ni Lowassa Lowassa
Badilini sare Kila kukicha ndo sera zenu
Kwa akili ya mtu mwenye akili timamu hawezi kukaa analinda kura,lazima tujiulize hivi wote tulinde kura zetu hicho kituo kitakuwaje?Je tutawekewa camera za kuona kinachoendelea huko ndani?Alichokipanga Mungu binadamu hatuwezi kukitengua,KAMWE.
ReplyDeletemnatuchanganya
ReplyDeleteJakaya ushauri wa bure uliingia madarakani kwa nguvu ya mtaandao. Wapiga kura wanahaki ya kukaa mita 200 ongeza Na Mia watakaa.ulisilete ubabe usiobebeka. Tulikubeba 2005 ,
ReplyDelete2015 si ya mbebo tena its people's power (ni nguvu ya isiyo Na mtaandao wala nini)
Watu waliochoka na ukilu timbal wa CCM. Unamaliza urais wako maliza kwa amani kama ulivyoingia usitishe watu kwakuwa una nguvu za dola.nguvu za dola zinamilikiwa Na umma
Acha uchaguzi uwe Huru Na amani kisiwe kisingizio uvunjifu wa amani kama wimbo wenu CCM kila kukicha
Tuachie tumchaguwe Na nani kwa mapenzi yetu
Kwa kauri zako hizi unambeba yule uliingia Na jina kamati kuu ya CCM ,nashukuru hata huko walikuzomeo, lakini hiii it's over over jakaya
Kama unataka kupoteza heshima yako itakuwa Mwaka huu
Tuachie Watanzania tuchague tunayemtaka
Na tuna mj uwa ni Nani
Huyu kiongozi ni mchochezi wa amani
ReplyDeleteMTANZANIA UNAPASWA UWE NA HESHIMA HATA KIDOGO UNAPOONGEA KWANINI TUFANANE NA MATAIFA MENGINE RAIS KIKWETE AMEFANYA MAMBO MENGI NA MAZURI, HEBU WEWE UNAYETUKANA HAPO JUU UWE NA HOFU YA MUNGU UKIINGIA WEWE MADARAKANI LEO UTAFANYA NINI. KWELI WATU WAZIMA HAO NI WAZAZI WAKO UNAWAAMBIA WAPUMBAVU? UKAWA VIPI JAMANI HATUWEZI KUEBDESHA NCHI KWA MTINDO HUU WA MATUSI. MUNGU WETU ATUSAMEHE. NAUMIA SANA SANA.
ReplyDelete