Sababu ya Shilole Kujichora Tattoo ya Nuhu Mziwanda Kwenye Ziwa Lake Imegundulika

STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametoboa siri ya kujichora tattoo yenye jina la mpenzi wake Naftari Mlawa ‘Nuh’ akisema alifanya hivyo ili kumpa imani mwanaume huyo kuwa anampenda sana.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Shilole alisema siku zote mpenzi wake hakuwa akiamini kama anampenda, licha ya ukweli kwamba naye alikuwa amechora tattoo yenye jina lake.

Nuh alikuwa haamini kama kweli nina mapenzi ya dhati kwake, niliamua kuchora tattoo ya jina lake na sasa ameamini nampenda, mapenzi yetu yameimarika kuliko mwanzoni, amejiona ni mtu muhimu sana kwangu, kwani hata mwanaume yeyote akiona nimejichora jina hili, lazima ashtuke na aone kwamba nina mtu tunayependana,” alisema.

GPL

Top Post Ad

Below Post Ad