SIRI IMEFICHUKA: Helkopta iliyomuua Filikunjombe na Wenzake Ilikuwa ni Mbovu Isiyofaa Kutumika Wala Kufanyiwa Matengenezo

Gazeti la The Star la nchini Kenya limeripoti kuwa chopa hiyo yenye uwezo wa kubeba kilo 1,000 na kuruka futi 20,000 ilithibitishwa na Taasisi ya Usalama wa Ndege kuwa mbovu, isiyofaa kwa matumizi wala matengenezo.

Dar es Salaam. Chopa iliyopata ajali katika pori la akiba la mbuga za Selous na kuua watu wanne akiwamo aliyekuwa mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe ni ya Makamu wa Rais wa zamani wa Kenya, Kalonzo Musyoka.

Msemaji wa Musyoka, Dennis Kavisu aliliambia gazeti la Daily Nation la Kenya kuwa chopa hiyo ni mali ya Musyoka aliyekuwa makamu wa rais wa zamani wa Kenya.
Gazeti la The Star la nchini Kenya limeripoti kuwa chopa hiyo yenye uwezo wa kubeba kilo 1,000 na kuruka futi 20,000 ilithibitishwa na Taasisi ya Usalama wa Ndege kuwa mbovu, isiyofaa kwa matumizi wala matengenezo

Chopa hiyo, yenye namba za usajili 5Y-DKK na namba za utengenezwaji 7027 Ecureuil ilikuwa ikitumiwa na Filikunjombe kwa kampeni zake za ubunge mwaka huu.
Wengine waliokufa katika ajali hiyo ni rubani, Kapteni William Silaa, Egid Nkwera na Plasdus Haule.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, chopa hiyo ni miongoni mwa nyingi zinazokodishwa kutoka Kenya na marais na wabunge wa nchini kwa kampeni. Kadhalika taarifa kutoka Kenya zinaonyesha Musyoka alinunua chopa hiyo mwaka 2013 baada ya Uchaguzi Mkuu na amekuwa akiikodisha ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi wa usalama na sheria wa Mamlaka ya Anga nchini (TCAA), Redemptus Bugomola hakutaka kuzungumza lolote kuhusu chanzo cha ajali ya chopa hiyo na mmiliki wake. “Bado nawasiliana na wenzangu wanaofanya uchunguzi, wakimaliza tutatoa taarifa rasmi kwenu kuhusu mmiliki na chanzo cha ajali,” alisema.

Katika mahojiano na gazeti hili wiki iliyopita, Mchunguzi Mkuu wa ndege wa Wizara ya Uchukuzi, John Nyamwihura alisema chanzo cha ajali za chopa ni makosa ya kibinadamu yanayosababishwa na rubani, hali ya hewa na mazingira ya chombo chenyewe

Mtandao wa usalama wa ndege unaeleza chopa mpya kama hiyo inagharimu kiasi cha Sh 7.3bilioni. Kwa kawaida chopa huuzwa zikiwa vipande na huunganishwa baada ya kufika zilikonunuliwa.
Kenya ina jumla ya chopa 400 zinazomilikiwa na watu binafsi wakiwamo wafanyabiashara na wanasiasa
.
MWANANCHI

Top Post Ad

Below Post Ad