Watanzania wenzangu!
Leo tarehe 29 October 2015, kwa kupitia Mgombea Mwenza wangu, Mh. Juma Duni Haji nimewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Tumeainisha kwenye malalamiko yetu, kutokuridhishwa kwetu na mwenendo na matukio mbalimbali, hususani, utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo halisi yaliyopatikana kwenye vituo vya kupiga kura, kama ifuatavyo.
• Upunguzwaji wa kura zangu
• Kuongeza kura kwa mgombea wa CCM
•Tunaendelea kukataa dhuluma hii dhidi ya matakwa ya wananchi, na jaribio la kutaka kubakwa kwa Demokrasia kunakooneka wazi kutokana na mwenendo wa Tume kuendelea kutangaza matokeo ya kura yasiyo ya kweli kwa kupoka ushindi wetu.
Aidha, kumekuwepo pia na uporaji wa ushindi kwa wagombea wa vyama vya UKAWA kwenye ngazi ya Ubunge na Udiwani
Kama tulivyoeleza jana takwimu zetu sisi zilionesha kwamba nilikua naongoza kwa zaidi ya 67%,na sasa tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10,268,795 sawa na asilimia 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima.
Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Naendelea kuwashukuru wananchi kwa imani yenu kwangu na kunichagua, MImi, pamoja na viongozi wenzangu tunaamini kuwa kuchezea Demokrasia ni kuvunja Amani, lakini sote tunatambua ni nyie watanzania ndio mnaoporwa haki yenu ya kupata mabadiliko, na viongozi mnao wahitaji, hivyo nitaendelea kuwa pamoja na watanzania wote kudai haki yenu kwa nguvu zote.
Tanzania kwa miaka mingi imefahamika kama kisiwa cha amani katika Afrika, tunashangaa leo kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikitanda kila mahali wakiwa na silaha za kivita mitaani kana kwamba uchagzui ni vita, hii ni kuwatisha wananchi ili wakubali kunyang’anywa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka, nina amini watanzania hatutakubali hali hiyo.
Lowassa, Edward Ngoyai.
29.10.2015
Babu rudi kijijini kachunge ng`ombe
ReplyDeleteLowawa urais huuwezi, acha ndoto za alinacha!
ReplyDeleteHatari jk huyo
ReplyDeleteMwenye nishani feki dunia nzima
Shame USA Na Europe sitisheni misaada yote kwa Tanzania
unaonekana wewe ni chizi kama mwenzio anayelalamikia matokeo, wakati magufuli akitembea kwa barabara kusaka kura yeye si aliona chopa ni dili? sasa analalamikia nini kama si wenda wazimu wakati kuna sehemu nyingi hakufika akaona kwa wanywa viloba ndiyo wanatosha???? kuwa makini usionekane boya
DeletePumbavu wewe sisi ndo watoa pesa kwa bajeti ya Tanzania
DeleteTunalipa kodi zetu lazima tuseme
Fisadi mkubwa wewe pamoja CCM wote
Wanasaikolojia wako wapi? nendeni kwa Lowassa mumsaidie jamani, laasivyo mzee wawatu atajinyonga.
ReplyDeletekwa mtu mwenye akili yeke timamu hawezi kumchagua Lowassa.
ReplyDeleteKatiba ya Tanzania nimbovu sana, ndio inafanya mambo yote haya kutokea. Ona zanzibar CCM walisema hawana imani na tume uchaguzi Umefutwa, Je ni kweli au walishaona wameshindwa Tayari....No DEMOCRACY ni kudanganyana tu hapa...
ReplyDeleteMfa maji haishi kutapatapa
ReplyDeleteNdio lishapigwa bao la mkono tena Lowasa kuwa raisi sahauu
ReplyDeleteJamani mlimsingizia TB Joshua katoa unabii kama Lowasa ndiyo atakuwa Rais sasa mmeumbuka
ReplyDeleteWW MANYWELE MEUPE LOWASA HIVI ZIMO AU NN NENDA KATIBIWE MARA UNAKUBALI
ReplyDeleteKUSHINDWA MARA WAKATAA KICHAA NN
Ndugu zangu Watanzania uchaguzi umekwisha, mshindi ametangazwa na sasa tuwaze juu ya maisha baada ya uchaguzi. Waswahili wana msemo wao unaosema "Asiyekubali kushindwa si mshindani" Nikuombe ndugu yangu Lowasa Ngoyai Edward kubali matokeo na epuka kutoa kauli ambazo zitaweza kuibua mihemuko kwa baadhi ya watu na kuanza kufikilia kukutafutia ushidi kwa nguvu na matokeo kutasababisha machafuko yatokee. Natambua wewe ni mmoja wa watu wanaoheshimika sana hapa nchini na nje ya nchi na ni moja ya senior leaders of Tanzania. Najua jinsi gani umeumia kuukosa Uraisi ulioutafuta kwa gharama kubwa ya fedha mathalani ulipotoa Bilioni 5 na kuwapa viongozi wa Chadema ili wakubali uwe mgombea, gharama za kampeni na nyonginezo kadha wa kadha. Naomba nikushauri kuwa ahana na Siasa ili iupate muda mwingi wa kupumzika kwani unaonekana hukubaliki katika kuiongoza Tanzania. Hebu fikili ulikatwa mwaka 1995, 2005 ulitamani ila ukamwacha rafiki yako kipenzi agombee kwa makubaliano uwe Waziri Mkuu, alikupa lakini ukashindwa kuiongoza serikali ukajiudhuru. Mwaka 2015 uliomba kuteuliwa kugombea Uraisi kupitia CCM lakini Halimashauri kuu ikakukata kwa mtazamo kuwa huna uwezo wa kuiongoza serikali husani unazo kashfa nyingi ambazo zilikupunguzia credit. POLE SANA NDUGU Lowasa.
ReplyDeletehaki lazima haijatendeka hata kidogo...CCM wezi wa kura hao...hawana lolote..kwanza hatuna imani kabisa na tume
DeleteIKULU NI MAHALI PATAKATIFU, HAINGII 'MCHAFU' MWENYE MAKANDO KANDO
DeletePPIIIIIIIIIPPOOOS, PWAAAAA
Familia wamsaidie huyu mzee jamani,mshaurini apumzike na aachane na hayo mambo ya siasa,naanza kuamini kwamba wako wanaomtumia kwa maslahi yao.Tunampenda kuwa nae bado,tukubali yaliyotokea.
ReplyDelete